Baada ya miamba ya soka Ujerumani kutolewa katika kampeni za kuwania taji hilo mwaka huu, imeomba radhi kwa mashabiki wake na kusema kuwa hawakucheza kama mabingwa.
Ujerumani ilitupwa nje ya mashindano hayo baada ya kuzaliwa mabao 2-0 na Korea ya Kusini katika dimba la Kazan nchini Russia.
Gazeti la udaku nchini Ujerumani la Bild liliandika 'Kichapo' baada ya mabingwa hao kushindwa kuvuka hatua ya makundi na kwamba ni miongoni mwa historia za kufadhaisha.
Timu hiyo ilionekana asubuhi ya Juni 28, katika Uwanja wa Ndege wa Vnukovo jijini Moscow ikijiandaa kurudi nchini Ujerumani
Mashabiki wa timu hiyo katika mtandao wa twitter wameitaka timu hiyo ichunguzwe kwa kina kuhusu namna ilivyocheza katika michuano hiyo.
Thomas Muller akiwa haamini kilichotokea Kazan Arena baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi |
Timu ya Taifa ya Ujerumani katika Uwanja wa Ndege wa Vnukovo, Moscow nchini Russia. |
Shabiki wa wa Ujerumani akishindwa kuvumilia na kujikuta akisononeka baada ya miamba hiyo kuzabuliwa mabao 2-0 na Korea Kusini hivyo kuyaaga mashindano hayo. |
Gazeti la udaku nchini Ujerumani la Bild liliandika 'Kichapo' baada ya mabingwa hao kushindwa kuvuka hatua ya makundi na kwamba ni miongoni mwa historia za kufadhaisha.
Timu hiyo ilionekana asubuhi ya Juni 28, katika Uwanja wa Ndege wa Vnukovo jijini Moscow ikijiandaa kurudi nchini Ujerumani
Mashabiki wa timu hiyo katika mtandao wa twitter wameitaka timu hiyo ichunguzwe kwa kina kuhusu namna ilivyocheza katika michuano hiyo.
0 Comments:
Post a Comment