Wednesday, June 27, 2018

Ripoti ya UN: Watoto 1,316 wauawa 2017, Saudia Arabia yashutumiwa

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Madhara yanawakumbwa wakati wa vita imetolewa huku Saudia Arabia ikishutumiwa vikali. 
Msanii wa Uchoraji Haifa Subay alichora picha ya watoto wawili akionyesha hisia zake kuhusu watoto wanaopata taabu kwenye vita ikiwa ni kampeni ya kunyamazisha mapigano jijini Sanaa. (Picha na Khaled Abdullah/Reuters).


Taifa hilo ambalo ni chanzo cha Uislamu duniani linashutumiwa vikali kuwa ndilo lilisababisha vifo na majeruhi kwa watoto katika vita nchini Yemen mwaka 2017. Ripoti hiyo imeweka wazi kuwa vifo vya watoto 1,316 vimetokea katika mataifa ya kiarabu. 


Mwaka 2015 Saudia Arabia na mataifa mengine ya Kiarabu yaliungana katika Kampeni za Kijeshi kuisaidia serikali ya Yemen dhidi ya waasi wa Houthi. Baadaye mataifa mengine yalijiondoa katika kampeni hizo baada ya kugundua kuwa yanalisaidia taifa hilo ambalo linasaidiwa na Marekani. 


Hata hivyo Saudia Arabia na Falme za Kiarabu (U.A.E) yakisalia katika kampeni hizo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliifikisha ripoti hiyo kwenye Baraza la Usalama Jumatatu usiku (25 Juni 2018). 


Ripoti hiyo imeongeza kuwa ilijiridhisha kuwa watoto 552 waliuawa miongoni mwao wa kiume 398 na wa kike 154. Aidha 370 ni watu wazima na 300 walijeruhiwa.

0 Comments:

Post a Comment