Watu 15 wamepoteza maisha na wengine 70 kujeruhiwa katika harakati za kujiokoa kwenye moto uliozuka na kuchoma soko moja nchini Kenya.
Moto ukiwaka katika soko la Gikomba asubuhi ya Juni 28, 2018 |
Mratibu wa kanda Kangethe Thuku alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba bado wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha moto huo.
Aidha moto huo umesababisha hasara kubwa ya mamilioni ya fedha baada ya kuteketeza kila kitu sokoni hapo.
Mashuhuda walisema moto huo ulitokea saa moja za asubuhi (EAT) katika soko la Gikomba jijini Nairobi.
Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali ya Taifa ya Kenyatta.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Thomas Mutie alithibitisha kupokea kwa wanaume 28, wanawake 42 na watoto 17.
Kituo cha Televisheni nchini humo cha NTV kimesema maelfu ya pesa yameteketea kwa moto bila kuweka wazi ni kiasi gani kutokana na moto kuteketeza bidhaa sokoni hapo.
Namna moto ulivyotekeza soko la Gikomba, jijini Nairobi |
0 Comments:
Post a Comment