Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Friday, April 28, 2017

Papa Francis na ziara ya saa 27 Cairo

Papa Francis akisalimia na Abdel Fatah al-Sisi baada ya kuwasili
Papa Francis akisalimiana na Sheikh Ahmed al-Tayeb
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amewasili katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri, kinachotambuliwa kuwa kituo kikuu cha elimu kwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni, kukutana na Imam Mkuu wa Misri Sheikh Ahmed al-Tayeb.
Awali Papa Fancis mwenye umri wa miaka 80, alikutana na Rais Abdel Fattah al-Sisi aliyemkaribisha kwa bendi ya kijeshi pamoja na mapadri waliojipanga kumsalimia Papa huyo.
Papa amesema ingawa ni safari ya siku mbili lakini ina umuhimu sana kwa kuwa ni safari ya umoja na udugu.

Leo la safari hiyo ni kutaka kuimarisha mahusiano na viongozi wa dini ya Kiislam katika wakati ambapo jamii ya kale ya Kikiristo nchini Misri inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislam (IS), wanaotishia kuitokomeza jamii hiyo.
Papa Francis akipunga mkono.

Tuesday, April 25, 2017

Wafanyakazi Wagonjwa wa muda mrefu Rufaa Mbeya wapata msaada

Wanamtandao walipozuru mojawapo ya nyumba ya Mfanyakazi wa Hospitali ya Kanda Rufaa Mbeya kumjulia hali baada ya utaratibu wa kuwatembelea kuanzishwa na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dkt. Godlove Mbwanji.
Katika kuhakikisha kuwa wagonjwa wa muda mrefu wanapata faraja, Umoja wa wanamtandao wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya umeanzisha utaratibu wa kuwatembelea wagonjwa hao kuwajulia hali kila mwezi.
Dkt. Godlove Mbwanji ambaye ni mwasisi wa mpango huo akiungana na wanamtandao hao wamewatembelea wagonjwa ambao ni wafanyakazi hospitalini hapo lakini kutokana na maradhi kuwashika kwa muda mrefu wameshindwa kufika maeneo ya kazi.
Wanamtandao hao waliopo kwenye mitandao ya kijamii waliunga mkono wazo la mwasisi huyo na kulifanyia kazi kwa vitendo ambapo walikutana majuma kadhaa yaliyopita na kuazimia kuwa na utaratibu huo ambao watakuwa wakipeleka vitu mbalimbali vya kuwatia moyo ikiwamo sukari, chumvi, sabuni na matunda.
Miongoni mwa wagonjwa wa kwanza kukutwa na utaratibu huo ni pamoja na mama Kaseko, Mr, Katembo, Mama Mwankotwa na Mama Pondo.
Kwa upande wa wagonjwa hao walikiri kushtushwa na ujio wa wanamtandao hao lililongozwa na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dkt. Mbwanji kwa kuendelea kuwajali na kuwathamini hali inayoonyesha hata walipokuwepo kazini hospitali hapo walikuwa wakiishi kwa upendo.
Kwa upande wake Dkt. Mbwanji alisema ni mara chache kuona mgonjwa akipewa kipaumbele hususani kwa wale wanaougua muda mrefu lakini alisukumwa kuanzisha utaratibu huo wa kuwatembelea wafanyakazi wa hospitali hiyo ambao ni wagonjwa wa muda mrefu na kwamba mpango huo ni endelevu.

Wanamtandao hao walisisitiza kuwa mpango ulianzishwa na Dkt. Mbwanji ni mfano kwa taasisi nyingine namna ya kuwajali wafanyakazi wao katika raha na shida.
Dkt. Mbwanji na mojawapo ya mgonjwa ambaye ni mfanyakazi wa Hospitali ya kanda Rufaa Mbeya hivi karibuni alipomtembelea kumjulia hali.

Cheyo: Muungano unapaswa kuimarishwa

John Cheyo
Mbunge wa zamani Bariadi Mashariki John Cheyo amesema ipo haja kwa Serikali kuboresha baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuwa ni kero kwa jamii  kwenye maeneo ya  Bara na Visiwani Zanzibar  ili kuimarisha Muungano.
Cheyo amesema katika kipindi cha miaka 53 ya muungano Serikali imefanya mambo mengi mazuri ingawa yanatakiwa kuimarishwa zaidi.
Cheyo amesema Muungano uliopo unapaswa kuwa wa kiundugu zaidi huku akiwataka wananchi wa Tanzangika na Zanzibar kusaidiana kwenye masuala mbalimbali bila kujali itikadi za kisiasa wala makabila yao.
Mwaka huu maadhimisho ya Muungano yatafanyika mjini Dodoma ambako sherehe zitafanyika Nyerere Square mjini humo ambapo jana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua maandalizi ya sherehe hizo hapo kesho.
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.
Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.
Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika,  kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusiana na muundo wa Muungano, baadhi wakitaka uwe wa zaidi ya serikali mbili, wengine serikali moja, wapo wanaotaka Tanganyika iwe kivyake na Zanzibar kivyake.

Friday, April 14, 2017

Miaka mitatu tangu kutekwa kwa Chibok Girls

MAIDUGURI, NIGERIA
Chibok Girls
Leo imetimia miaka mitatu kamili tangu kundi la kigaidi la Boko Haram lilipowateka wasichana zaidi ya 270 kutoka shuleni kwao katika kijiji cha Chibok kaskazinimashariki mwa Nigeria.
Katika idadi hiyo, wasichana kadhaa walifanikiwa kutoroka au kuachiwa huru, lakini wengine 195 bado hawajapatikana. Msemaji wa rais wa Nigeria Garba Shehu amesema serikali inajadiliana kwa msaada wa mataifa na mashirika ya kigeni ili kufanikisha kuachiwa kwa wasichana wanaoendelea kushikiliwa na kundi la Boko Haram.
Shehu amesema wasichana 21 walioachiwa kwa msaada wa shirika la misaada la Msalaba Mwekundu ICRC na maafisa wa serikali ya Uswisi, na kuongeza kuwa ICRC na serikali ya Uswisi wanaendelea kuunga mkono majadiliano hayo.

Boko Haram iliwateka wanafunzi 276 kutoka shule ya sekondari ya serikali mjini Chibok Aprili 14, 2014.

Tuesday, April 11, 2017

Wanamtandao waunga mkono juhudi za Dkt. Mbwanji Mbeya

Wanamtandao katika picha ya pamoja wakati wa kupeleka mifuko 11 ya saruji kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Dkt. Mbwanji
Wahenga walisema Uchungu wa Mwana Ajuaye Mzazi, pia wahenga hao walisema Umoja ni Nguvu; hii imejidhihirisha kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji kujitolea kujenga wodi moja kwa ajili ya watoto.
Chanzo chetu kilitujuza kuwa kilichomsukuma Dkt. Mbwanji ni baada ya kuona ongezeko la wagonjwa hususani watoto ni kubwa ndipo alipoamua kujenga wodi maalum.
Hata hivyo kundi moja la Watu wanaojihusisha na mitandao ya kijamii mkoani humo lilipoona juhudi za mtalaamu huyo likajichangisha mifuko 11 ya saruji ili kuunga mkono juhudi hizo.
“Ujenzi bado unaendelea wa wodi hiyo. Tunaamini ikishamalizika itakuwa msaada mkubwa sana kwa watoto wanaotibiwa katika hospitali yetu,” kilisema chanzo hicho
Hadi sasa bado blog hii haijapata ujenzi huo utagharimu kiasi gani kwa mwenye maelezo ya kina unaweza kutuma katika namba ifuatayo. 
+255-(0)-768 096 793




Saturday, April 1, 2017

Said Makora atupiwa lawama na madaktari

BAADHI ya Madaktari wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya kwa Jamii Muhimbili, wamemlalamikia Kaimu Mkurugenzi, Said Makora kwamba hana uwezo wa kuongoza kitengo hicho kwa vile hana uwelewa wa fani ya Afya.
Mwenyewe ajibu, kuwa hata Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, hana elimu ya afya lakini anaongoza Maprofesa na Madaktari.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wataalam hao walisema kuna haja sasa kitengo hicho kuongozwa na watu waliyosomea fani hiyo ya afya.
Madaktari hao walifikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mkurugenzi huyo amekuwa akikiletea aibu kitengo hicho kutokana na kushindwa kijibu masuala yanayohusu afya pindi anapokutana na wahisani.
"Unajua Kaimu Mkurugenzi wetu hana uwezo wa kutambua masuala ya afaya kwani yeye ni msomi wa Chuo Kikuu hususan masuala Mawasilano kwa umma pamoja na yote pia uhusiano wake kikazi na wataalamu siyo wa kuridhisha zaidi ya manyanyaso,"alisema mmoja wao.
Hata hivyo, walisema kuteuliwa kwa mkurugenzi huyo kumetokana na nguvu kubwa iliyotumika kutoka kwa baadhi ya vigogo wa walioko katika wizara hiyo, ambao ndiyo wanaompa kiburi cha kuwanyanyasa madaktari hao.
Makora, alisema kuwa malalamiko hayo hayana msingi bali wanapaswa kutambua kuwa suala la uongozi na udaktari ni vitu viwili tofauti.
"Ummy mwalimu ana digiree mbili za sheria lakini anawaongoza wataalamu wa afya kama vile Profesa Bakari wa magonjwa ya binadamu na Dkt. Mpoki Lisubisya mtalamu wa magonjwa ya usinizi, kwa hiyo mimi ni kiongozi,” alisema Makora.
Alisema, kutokana na mazingira hayo basi ingekuwa anayestahili kuwa Waziri angekuwa Prof Bakari, Naibu Waziri Prof Lisubisya huku Ummy akipaswa kuwa Katibu, hao watu wamezoea kulalamika.
Alisema wanaojua anayefaa kuongoza katika Idara fulani ni serikali na Idara ya Utumishi na isitoshe yaye ameaminiwa na ofisi ya Katibu Mkuu.