Kijiji cha
Makiwaru kimepata Maji ya Kisima kwa
ajili ya shughuli za kila siku ikiwamo matumizi ya ndani kama kupika, kuoga,
kufua na kadhalika.
Changamoto ya muda mrefu imefikia ukomo baada ya kijana mwenye umri wa miaka 26
anayefahamika kwa jina la Eric Salema mwenyeji wa kijiji hicho kilichopo
Magharibi mwa Mji mdogo wa Sanya Juu mkoani Kilimanjaro, kutimiza ndoto yake
kupitia mradi wa Dream Maker, Betpawa
kwa manufaa ya wanakijiji hao.
“BetPawa walijitolea kuja kunichimbia kisima cha maji, kwa
ajili yetu sisi wananachi, ukweli ni kwamba yatatusaidia sisi kama mwananchi wa
kijiji hiki, kutatua changamoto yetu kubwa tuliyokuwa nayo hapa. Changamoto ya
maji ipo kubwa maji mabomba ya maji yapo lakini upatikanaji wa maji ni wa
kusuasua, inaweza kupita wiki hatupati maji kabisa kupitia mradi huu unakwenda
kutatua changamoo hiyo,” anasema Eric Salema.
Meneja Masoko wa Betpawa Bi. Borah Ndanyungu anasema Mradi wa
Dream Maker ni njia ya kurudisha kitu kwa umma bila kujali ni mteja wa
kampuni hiyo au la.
“Tulipata ndoto zaidi ya 15,000 lakini ndoto ya Eric Salema
ilitugusa zaidi, ndoto ambayo ni endelevu ambayo inaigusa jamii moja kwa moja
na sisi kama kampuni tunatumia muda takribani mwezi ikiwa na tim u ya watu
mbalimbali kupitia hizi ndoto za wananchi ambazo huziwasilisha kwetu,” anasema
Borah Ndanyungu.
Eric anasema ndoto yake ilikuwa kweli baada ya kutembelea
mtandao wa Betpawa ambao uliweka namna ya kufikia ndoto ni muhimu kuwasilisha
wazo ambalo litakuwa na manufaa kwa wananchi.
Mhandisi wa Kisima hicho Injinia John Francis Madaraka
anasema uzinduzi wa kisima hicho ambacho kimegharimu kiasi cha shilingi mil. 24
za Tanzania utahudumia wakazi kati ya 4000 hadi 6000.
“Tumechimba kina cha mita 90 maji ni safi na salama, yamesha
thibitishwa tuliyapeleka Idara ya Maji
wakayapima yanafaa kwa matumizi ya binadamu, ambapo kisima hicho kina
uwezo wa kuhudumia watu kati ya 4000 hadi 6000,” anasema Injinia Madaraka.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Makiwaru Jackson
Moye anasema changamoto ya maji kijijini hapo imekuwapo kwa muda sasa lakini
ujio wa kisima hicho umepunguza huku akisifu juhudi za kijana Eric Salema.
“Kwa kipindi cha kiangazi maji huwa madogo, wananchi
hulazimika kutafuta maji vituo vingine na wakati mwingine usiku wakitafuta
maji, Mradi huu ambao umetufikia katika kijiji hiki, utakwenda kupunguza changamoto
ya maji, tunashukuru sana kwa hiki kilichofanyika husasan kwa kijana wetu kwa
kuchagua mradi huu uletwe hapa nyumbani kwa wazazi wake,” anaongeza Moye.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kijiji
cha Makiwaru kina wakazi 3425 hivyo uwepo wa kisima hicho chenye urefu wa mita
90 utaondoa kero ya wakazi wa kijiji hicho kusafiri umbali mrefu kutafuta maji.
Mradi wa Dream Maker katika msimu wake wa pili umegharimu
kiasi cha shilingi mil. 600 kutimiza ndoto 20 zilizochaguliwa kati ya 10,000
zilizowasilishwa Betpawa kwa njia ya mtandao.
0 Comments:
Post a Comment