Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Saturday, August 31, 2024

Chuo cha Montessori, Ushirika wa Neema, Moshi chaadhimisha miaka 154 ya kuzaliwa

Maria Tecla Montessori, 1870-1952 (Picha na Mtandao/Luce)

 “Niliondoka Italia mnamo mwaka 1934, wakati ambao shule zote nilizoanzisha zikiwa zimefungwa, Niliishi uhamishoni barani Ulaya mpaka mwaka 1939 na baadaye nikaenda kuishi nchini India kwa miaka saba (7) kwa miaka mitano nilitiwa kizuizini kama adui wa Waitaliano, sikuweza kusafiri, lakini raia wa India walinijia siku moja na nikafanikiwa kuwafundisha walimu 1500.”

Maria Tecla Artemisia Montessori alikuwa akizungumza na vyombo vya habari nchini Italia akitokea India mnamo mwaka 1940.

Wanafunzi wa Chuo cha Montessori, Ushirika wa Neema mjini Moshi wakiwa na Mkuu wa Chuo hicho Sister Christine Nakey katika kuadhimisha miaka 154 tangu kuzaliwa kwa Dkt. Maria Montessori mnamo Tarehe 31 Agosti 2024. (Picha Na. JAIZMELA/Kija Kisena)

Agosti 31, 1870 katika mji wa Chiaravalle uliopo katika mkoa wa Marche nchini Italia alizaliwa mwanamke wa kwanza nchini humo kuwa daktari wa magonjwa ya watoto na magonjwa ya akili Maria Montessori.

Wakati akizaliwa katika mji huo hakuna aliyewahi kudhani kama siku moja Maria Montessori angekuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliowahi kuwepo ulimwenguni na kutoa msaada mkubwa sana hadi sasa.

Katika ugunduzi wake alibaini kuwa watoto waliovia akili wanaweza kufunzwa kwa kutumia vifaa vya kuchezea wanavyovipenda. Aliamini kuwa tatizo la kuvia akili ni la kielimu na sio la tiba.

Maria Montessori aliamini kuwa elimu ya mtoto ni lazima ianze mapema sana kwa sababu umri wa mtoto  kati ya kuzaliwa  hadi miaka sita ni muhimu sana kwa ujenzi wa haiba yake.

Ili mtoto aweze kujifunza kwa ufanisi zaidi ni muhimu kwa mzazi au mwalimu kutumia michezo na vitendo vinginevyo katika kufundisha,hii itamsaidia mtoto katika kujifunza kujifunzia stadi mbalimbali za utendaji .

Maria Montessori   anajulikana sana kwa kuwa mtu aliyeanzisha njia ya kuwafundisha watoto wadogo.

Maria Monterssori ameacha alama duniani ikiwamo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambako Chuo cha Mafunzo ya Ualimu Montessori Ushirika wa Neema kilichopo Manispaa ya Moshi, kimeadhimisha miaka 154, tangu kuzaliwa kwa Dkt. Maria Montessori.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Chuo hicho Sister Christine Nakey, amewataka wazazi na walezi  kuwajali watoto wenye changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwemo wenye ulemavu kutokana na ukweli kuwa na wao wana nafasi katika kuchangia maendeleo ya nchi.

Wito umetolewa kwa Wizara ya Elimu nchini Tanzania kuwa na kitengo ambacho kitatumia mitaala ya mwanzilishi Maria Montessori katika kujifunza.

Kwa upande wao wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho wamesema elimu ya Montessori inaenda sambamba na vitendo hivyo kumjenga mwanafunzi kujiamini na kupambana na mazingira yanayomkabili hata baada ya kuhitimu mafunzo.

Maria Montessori atazidi kukumbukwa na kuenziwa kwani alipendekeza mwalimu atumie vifaa vingi katika ufundishaji, vifaa hivyo viwe ni vile vinavyokuza tabia ya udadisi na ugunduzi,vinavyompa nafasi ya utendaji na vinavyomwezesha kufanya majarabio,kutatua vikwazo,ujasiri,kuuliza na kujibu maswali,kupenda kufaulu, kujiendeleza na kumpa msukumo wa kujitegemea katika utendaji.

Alifariki dunia mnamo Mei 6, 1952 magharibi mwa Uholanzi katika mji wa Noordwijk  akiwa na umri wa miaka 81 na alizikwa huko huko Noordwijk.










Friday, August 30, 2024

Wednesday, August 28, 2024

Wamajumuhi wa Afrika mjini Moshi waadhimisha kuzaliwa kwa Marcus Garvey (1887-1940)

Marcus Garvey (1887-1940)

 Wamajumuhi wa Afrika mjini Moshi wameadhimisha miaka 137 ya kuzaliwa kwa Mwanaharakati wa Haki za Watu Weusi Marcus Garvey.

Maadhimisho hayo yamefanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mnamo Agosti 17, 2024 yakiwaleta pamoja wamajumuhi wengine kutokaTanzania na  Amerika hususani Jamaica, Trinidad & Tobago na Canada.

Akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo mwenyeji wa Wamajumuhi hao Rasta Gasper Shirima anasema wanaendelea kushikilia falsafa za Garvey licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki ikiwamo ukosefu wa maarifa kwa watu wa Afrika Mashabiki kuhusu umajumuhi wenyewe wa Kiafrika.

Rasta Shirima anaongeza kusema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejitahidi kuwapa eneo katika Manispaa ya Moshi kwa ajili ya kutoa maarifa hayo Bure licha ya mwendo wa kinyonga katika kubadilisha mitaala ya Elimu na kuweka umajumuhi wa Kiafrika.

Suala la waafrika walio nje ya nchi zao wanaofahamika kwa jina la Diaspora lilikuwa mjadala mrefu huku wakitaka kujua hatua zimefikia wapi kuwafikia viongozi wa serikali na wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutoa mwanya wa kubadilisha Sheria.

Watanzania wenyewe wanasemaje kuhusu umajumuhi wa Kiafrika na jamii inawatazamaje wanapojifunza.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Tiba Asili kutoka nchini Jamaica Michael Jocko amewataka watanzania kuwa na nidhamu ya chakula ili kutunza Afya zao na kuwa na maisha marefu.

Marcus Garvey alizaliwa Jamaica mwaka 1887. Kwamba mweusi huyu wa ngozi aliyewataka Waafrika kujivunia Uafrika wao, alizaliwa katika bara la Amerika Kusini ni kielelezo cha historia chungu ya ujenzi wa ubepari. Ubepari wa Ulaya ulijengwa katika msingi wa uporaji wa ardhi kutoka kwa wenyeji wa Amerika, na uporaji wa nguvu-kazi kutoka Afrika. Hadi kufikia mwaka 1800, mathalani, idadi ya wazungu kisiwani Jamaica ilikuwa ni ishirini na moja elfu huku Waafrika waliogeuzwa watumwa wakiwa ni laki tatu. “Watumwa” hao walitumika kuzalisha miwa/sukari ambayo ilisafirishwa kwenda Uingereza.

Wakati Garvey anazaliwa, biashara ya utumwa ilikuwa imekomeshwa huko Amerika, lakini Waafrika hawakuonekana kama binadamu kamili: waliendelea kubaguliwa, kunyanyaswa na kunyonywa.

Garvey aliuona ubaguzi huo tangu akiwa mdogo nchini Jamaica. Haishangazi basi, mapambano yake yalikuwa ni ya kupinga ubaguzi wa rangi. Baada ya kusafiri na kufanya kazi katika nchi mbali mbali za Karibiani, na baadaye Uingereza, Garvey alikwenda Marekani mwaka 1916. Ni huko Marekani ambako taasisi aliyoianzisha, ijulikanayo kama UNIA (Universal Negro Improvement Association) ilipata wanachama na wafuasi wengi.


























Wednesday, August 21, 2024

Dream Maker, Betpawa yatimiza ndoto ya Eric Salema kupata Kisima cha Maji Makiwaru

 

Kijiji cha Makiwaru  kimepata Maji ya Kisima kwa ajili ya shughuli za kila siku ikiwamo matumizi ya ndani kama kupika, kuoga, kufua na kadhalika.

Changamoto ya muda mrefu imefikia ukomo  baada ya kijana mwenye umri wa miaka 26 anayefahamika kwa jina la Eric Salema mwenyeji wa kijiji hicho kilichopo Magharibi mwa Mji mdogo wa Sanya Juu mkoani Kilimanjaro, kutimiza ndoto yake kupitia mradi wa Dream Maker, Betpawa  kwa manufaa ya wanakijiji hao.

“BetPawa walijitolea kuja kunichimbia kisima cha maji, kwa ajili yetu sisi wananachi, ukweli ni kwamba yatatusaidia sisi kama mwananchi wa kijiji hiki, kutatua changamoto yetu kubwa tuliyokuwa nayo hapa. Changamoto ya maji ipo kubwa maji mabomba ya maji yapo lakini upatikanaji wa maji ni wa kusuasua, inaweza kupita wiki hatupati maji kabisa kupitia mradi huu unakwenda kutatua changamoo hiyo,” anasema Eric Salema.

Meneja Masoko wa Betpawa Bi. Borah Ndanyungu anasema Mradi wa Dream Maker ni njia ya kurudisha kitu kwa umma bila kujali ni mteja wa kampuni  hiyo au la.

“Tulipata ndoto zaidi ya 15,000 lakini ndoto ya Eric Salema ilitugusa zaidi, ndoto ambayo ni endelevu ambayo inaigusa jamii moja kwa moja na sisi kama kampuni tunatumia muda takribani mwezi ikiwa na tim u ya watu mbalimbali kupitia hizi ndoto za wananchi ambazo huziwasilisha kwetu,” anasema Borah Ndanyungu.

Eric anasema ndoto yake ilikuwa kweli baada ya kutembelea mtandao wa Betpawa ambao uliweka namna ya kufikia ndoto ni muhimu kuwasilisha wazo ambalo litakuwa na manufaa kwa wananchi.

Mhandisi wa Kisima hicho Injinia John Francis Madaraka anasema uzinduzi wa kisima hicho ambacho kimegharimu kiasi cha shilingi mil. 24 za Tanzania utahudumia wakazi kati ya 4000 hadi 6000.

“Tumechimba kina cha mita 90 maji ni safi na salama, yamesha thibitishwa tuliyapeleka Idara ya Maji  wakayapima yanafaa kwa matumizi ya binadamu, ambapo kisima hicho kina uwezo wa kuhudumia watu kati ya 4000 hadi 6000,” anasema Injinia Madaraka.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Makiwaru Jackson Moye anasema changamoto ya maji kijijini hapo imekuwapo kwa muda sasa lakini ujio wa kisima hicho umepunguza huku akisifu juhudi za kijana Eric Salema.

“Kwa kipindi cha kiangazi maji huwa madogo, wananchi hulazimika kutafuta maji vituo vingine na wakati mwingine usiku wakitafuta maji, Mradi huu ambao umetufikia katika kijiji hiki, utakwenda kupunguza changamoto ya maji, tunashukuru sana kwa hiki kilichofanyika husasan kwa kijana wetu kwa kuchagua mradi huu uletwe hapa nyumbani kwa wazazi wake,” anaongeza Moye.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kijiji cha Makiwaru kina wakazi 3425 hivyo uwepo wa kisima hicho chenye urefu wa mita 90 utaondoa kero ya wakazi wa kijiji hicho kusafiri umbali mrefu kutafuta maji.

Mradi wa Dream Maker katika msimu wake wa pili umegharimu kiasi cha shilingi mil. 600 kutimiza ndoto 20 zilizochaguliwa kati ya 10,000 zilizowasilishwa Betpawa kwa njia ya mtandao.







Friday, August 9, 2024

Afariki Dunia akijaribu kuokoa simu kisima cha mafuta Moshi


Kijana aliyefahamika kwa jina la Shalom Tarimo (21) amefariki Dunia Leo adhuhuri wakati akifanya Usafi katika kituo cha Mafuta cha Uhuru Peak mjini Moshi mkoani Kilimanjaro

Tarimo ambaye alikuwa kijana wa kazi amefariki Dunia kwa kutumbukia kwenye kisima cha mafuta wakati akijaribu kutoka simu iliyomponyoka mfukoni.

Jeshi la Zimamoto na uokoaji lilifika na kuchukua takribani saa moja kutoa mwili wa marehemu katika kisima hicho kilichopo katika kituo cha Mafuta cha Total Energies cha Uhuru Peak.


Mchungaji aliyefariki kwa ajali Kimashuku Moshi kuzikwa leo

Aliyekuwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kimashuku Kantante Munisi (42) wilayani Hai mkoani Kilimanjaro anatarajia kuzikwa hii leo na umati wa watu waliokusanyika kwa ajili ya kumsindikiza marehemu huyo, kijijini kwao Kisamo, Moshi Vijijini

Mchungaji Kantante alifariki Dunia kwa ajali ya basi  siku chache zilizopita baada gari la abiria Kampuni ya Shabiby T 142 EGM kuacha njia na kulifuata gari la Mchungaji huyo wakati akienda kanisa kuhudumu

Ibada ya maziko inaendelea katika Usharika wa kanisa la Kisamo, Moshi Vijijini.