Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Saturday, September 23, 2023

LIGI YA KIKAPU KILIMANJARO 2023: MOCU watwaa ubingwa, watoa MVP

 

MOSHI, TANZANIA.

Timu ya Kikapu ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuibamiza Wakuda  kwa pointi 100-82 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika dimba la Ushirika mjini Moshi.


Katika mchezo huo wa fainali kulishuhudiwa ufundi mwingi huku MOCU ikionyesha umahiri mkubwa katika robo ya kwanza na ya mwisho ya mchezo huo.


Licha ya Wakuda kutawala zaidi katika robo ya pili na ya tatu ya mchezo lakini hawakuweza kuzuia kasi ya MOCU ambayo imetoa mcheza bora wa mashindano hayo mwaka huu.


Mashabiki wa kikapu mkoani Kilimanjaro walisema msimu wa ligi mwaka huu ulikuwa wa kuvutia na umetoa ari na hamasa kujiandaa kwa msimu mwingine.


Kwa upande wao Wakuda walisema ubora wa MOCU ndio uliowafanya washindwe kutoboa na kubeba taji hilo mwaka huu licha ya kupita katika hatua za awali kwa kishindo.


Daniel Kayusi wa timu ya kikapu ya MOCU ameibuka mchezaji bora wa mashindano mwaka huu akifikisha pointi 249 nyuma ya mfungaji bora wa msimu huu kutoka Wakuda aliyefikisha pointi 255 Noel Joseph .


Mratibu wa Mashindano hayo Emmanuel Constantine alisema msimu wa mwaka huu licha ya changamoto zake lakini umekuwa ni msimu bora na ametoa wito kwa msimu ujao timu kujitokeza kwa wingi kushiriki.


Ubingwa wa kikapu kwa MOCU unakuja baada ya kufanya vizuri katika hatua za awali ambapo ameweka rekodi ya kushinda michezo yote iliyochezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini katika ligi ya timu saba zilizoshiriki msimu huu.


Timu nyingine zilizoshiriki ni VTI, KCMC, Don Bosco, Kijiji Mashujaa na Hai.