Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Saturday, January 12, 2019

Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Zanzibar inaadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi kwa sherehe zinazofanyika kwa mara ya kwanza kisiwani Pemba tangu alipoingia madarakani Rais Ali Mohammed Shein.

ILIKUWAJE?
Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. 

Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi wa meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. 

Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. 

Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi. Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. 

Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. 

Wakati mfalme mpya, Jamshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar. 

Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. 

Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu. Na Ilipofika Aprili 26, 1964 liliungana na Tanganyika kutengeneza kile kinachofahamika kwa sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Sasa ni miaka 55 tangu mapinduzi hayo yafanyike. Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Dkt. Ali Mohamed Shein ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo hapo hii leo. Akizungumza na wanahabari. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa pili Mohamed Aboud Mohamed alithibitisha uwepo kiongozi huyo na viongozi wengine wan chi mbalimbali akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli. 

Aidha Dkt. Shein amewasamehe wafungwa 12 walioonyesha nidhamu wakiwa jela.

Kauli mbiu mwaka huu ni “Mapinduzi yetu ni Umoja wetu tuyalinde kwa maendeleo yetu.”




Friday, January 11, 2019

AFC Asia Cup: India yazabuliwa 2-0 na wenyeji U.A.E


Licha ya kuanza mchezo wa kwanza kwa ushindi lakini jana India ilishindwa kutamba mbele ya wenyeji wa michuano ya soka kwa mataifa ya Asia Falme za Kiarabu  baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 (kwa mtungi). 

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Zayed Sports City kulishuhudiwa wenyeji hao wakigusa nyavu katika dakika ya 41 ya mchezo pale Khaflan Mubarak alipofumua mkwaju wa nguvu kwa kutumia mguu wake wa kulia upande wa kulia juu baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ali Ahmed Mabkhout. 

Bao hilo lilikuja baada ya muda wa mashambulizi na kosakosa nyingi katika lango la India. Bao la pili lilifungwa na Ali Ahmed Mabkhout kwa mguu wa kulia akipokea pasi ya kiungo Ali Hassan Salmin kisha kuupiga upande wa kushoto chini  na kumwacha mlinda mlango Gurpreet Singh Sandhu.  

Mchezo mwingine wa kundi A kulishuhudia Bahrain ikishindwa kutamba mbele ya Thailand baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 mtanange uliochezwa jijini Dubai. Kundi B liliendelea tena jana kwa Jordan kuizabua Syria kwa mabao 2-0 mjini Al Ain. 

Leo hatua ya makundi itaendelea kwa Australia kuikabili Palestina katika mchezo wa kundi B mtanange utakaochezwa katika dimba la Rashid jijini Dubai utaanza saa 8:00 mchana Australia ilianza kampeni zake kwa kichapo hivyo leo itakuwa ikitaka kurudhisha makali yake. 

Kundi C litaingia vitani kuanzia za 10:30 jioni jijini Abu Dhabi na Al Ain pale Ufilipino ya kocha raia wa Sweden Sven-Goran Eriksson itakapoikabili China katika mchezo unatarajiwa kuwa mkali. Pia Jamhuri ya KYRGYZ itapambana vikali Korea Kusini.  

Thursday, January 10, 2019

Jaguar Land Rover kupunguza wafanyakazi

Watengenezaji wakubwa wa magari nchini Uingereza wa Jaguar Land Rover wanajiandaa kupunguza maelfu ya ajira wakati ambao kampuni hilo linakutana na uuzaji mdogo wa magari yake nchini China. 

Sababu nyingine inayotajwa ya kupunguza wafanyakazi wa kampuni hilo ni kushuka kwa uuzaji wa mafuta ya dizeli barani Ulaya. Waziri wa Biashara wa Uingereza Greg Clark amesema mapema leo kwamba kutojiondoa katika umoja wa Ulaya kutaongeza matatizo makubwa na gharama za uendeshaji zitapanda. 

Kampuni hilo limepoteza kiasi cha zaidi ya trilioni moja kati ya Aprili na Septemba mwaka 2018 na mpaka sasa imeshapunguza ajira 1,000. 

Pia imefunga kiwanda chake cha Solihul kwa majuma mawili huku ikitangaza uzalishaji wa kiwanda cha Castle Bromwich kitapaswa kufanya kazi mara tatu kwa juma.

Tshisekedi atangazwa rasmi Rais wa DR Congo

Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo ametangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na tume ya uchaguzi baada ya kuchelewesha matokeo ya uchaguzi kwa muda mrefu. 

Jana kabla ya kutangaza matokeo hayo Polisi wa kuzuia fujo wakiwa na mizinga ya maji ya kuwasha na magari ya kijeshi waliyazunguka makao makuu ya tume ya uchaguzi kabla ya kutangazwa.  

Matokeo hayo ambayo yametangazwa yamepingwa vikali na Martin Fayulu ambayo alionekana kupata uungwaji mkono wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi wa Desemba 30.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Corneille Nangaa ametangaza kuwa Tshisekedi ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 38.57 ya kura zaidi ya milioni 18 zilizopigwa.  

Tshisekedi mwenye umri wa miaka 55 amepata kura milioni saba zaidi ya zile za Fayulu ambaye amepata kura milioni 6.4; Emmanuel Ramazani Shadary ambaye alichaguliwa na Joseph Kabila kuwania nafasi hiyo ameshika nafasi ya tatu kwa kura milioni 4.4 

Kwa upande wake Tshisekedi ameahidi kurudisha utawala wa sheria, kupambana na magenge ya rushwa na kurudisha amani katika eneo la mashariki lenye utajiri mwingi wa madini. 

Uchaguzi huo unakuwa wa kwanza wa kidemokrasia tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mwaka 1960 kutoka kwa Ubelgiji na Kabila anatarajiwa kuondoka ikulu baadaye mwezi huu.

Wednesday, January 9, 2019

Mahakama yatupilia mbali kesi ya mapitio ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao


Mahakama Kuu kanda ya Mtwara imetupilia mbali kesi ya kutaka mapitio ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao iliyofunguliwa na Baraza la Habari Tanzania MCT, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu 

LHRC na Muungano wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC). Katika kesi hiyo washtakiwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu. 

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Wilfread Ndyansobera. Katika maamuzi yake Jaji Ndyansobera amesema kwamba maombi ya wapeleka maombi hayana uzito na kwamba walalamikaji wameshindwa kuthibitisha  jinsi gani Kanuni hizo zitakavyoathiri haki za msingi za walalamikaji katika masuala ya uhuru wa habari na mawasiliano ya mitandaoni.

Jaji wa kesi hiyo amesema mahakama imekubaliana na hoja za  Mawakili wa Serikali kuwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni zimetungwa kwa mujibu wa sheria. Kesi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Septemba 4, 2018.

Sunday, January 6, 2019

AFC Asia Cup: India yaanza vema hatua ya makundi

Sunil Chhetri akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao dhid ya Thailand January 6 mwaka huu
Kundi A limeanza kampeni zake za kuwania taji la soka kwa  Mataifa ya Asia mwaka huu huku India ikiizabua Thailand kwa mabao 4-1. Sunil Chhetri mwenye miaka 34 alifunga mara mbili katika ushindi huo. 

Ushindi huo ni wa kwanza mkubwa kwa India baada ya miaka 55 katika mechi za ufunguzi kwenye michuano hiyo. Mabao mengine yalifungwa na Anirudh Thapa na Jeje Lalpekhlua Katika mechi ya Ufunguzi siku ya Jumamosi wenyeji wa mashindano hayo Falme za Kiarabu waligawana pointi na Bahrain kwa sare ya bao 1-1. 

Bao lililofungwa kwa mkwaju wa penati dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo huo na Ahmed Khalil limewafanya wenyeji hao kuiangazia India watakaposhuka dimbani Januari 10. Kundi C linaanza kampeni zake leo kwa China kucheza na Jamhuri ya Kyrgyz mjini Al Ain. Kikosi cha China kinachonolewa na Marcelo Lippi aliywahi kuinoa miamba ya soka Italia na kutwaa taji la Dunia mwaka 2006 kitajiuliza leo. 

Kocha huyo amekuwa na mafanikio makubwa katika soka la Asia kwani mwaka 2013 aliipa taji ligi ya mabingwa klabu ya Guangzhou Evergrande. Lippi amekaririwa akisema wanachotaka ni kuwa na matokeo mazuri ili kuweza kusonga mbele.

Saturday, January 5, 2019

Djokovic ashindwa kutinga fainali Qatar Open 2019

Mchezaji wa tenisi namba moja ulimwenguni Novak Djokovic ameshindwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya wazi ya tenisi ya Qatar akipata kichapo cha kustaajabisha kutoka kwa mchezaji wa tenisi namba 24 kwa ubora duniani Roberto Bautista Agut raia wa Hispania. 
Roberto Bautista Agus akishangilia baada ya kumtandika Djokovic.

Djokovic anayejiandaa na michuano ya wazi ya Australia alishindwa kufurukuta zaidi ya saa mbili na nusu akipoteza kwa seti 6-3 6-7(8-6) 6-4. Hii ni mara ya pili Agut anamtandika Djokovic katika maisha yake ya tenisi na mara zote amemzabua katika nusu fainali. 

Akiwa namba moja kwa ubora duniani Djokovic alishindwa kufurukuta mbele ya Agut Oktoba 2016 katika michuano ya Shanghai Masters. Nyota huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 30 alisema ataukumbuka mchezo huo katika maisha yake.