Thursday, October 25, 2018
TaSUBa ni nini?
TaSUBa ni Wakala wa serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa
sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2009, kupitia tangazo la Serikali Na. 220 la Novemba 2, 2007.
Taasisi hii inatokana na kilichokuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho
kilianzishwa mwaka 1981 baada ya kuvunjwa kwa kikundi cha Sanaa za Maonesho cha
Taifa mwaka 1980.
Rashidi M. Masimbi ndiye aliyekuwa mkuu wa kwanza wa chuo cha
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kabla hakibadilishwa na kuitwa TaSUBa kuanzia mwaka
1981-1987 akafutiwa na J. Mwakipesile (1987-1987), R. Mashimbi (1989-1997), P.
Nyambasi (1997-2007) na Juma A. Bakari (2003-2007).
Baada ya kuundwa kwa Wizara ya Utamaduni mwaka 1962,
kilianzishwa kikundi cha Sanaa za Maonesho cha Taifa ambacho kilianza na fani
ya ngoma (1963), Sarakasi (1969) na Tamthilia (1974). Kazi kubwa ya Kikundi
hiki ilikuwa kufanya maonesho sehemu mbali mbali nchini ili kukuza mwamko wa
kuupenda na kuutukuza utamaduni wa Watanzania ambao mkoloni alijitahidi kwa
nguvu zake zote kuukandamiza.
Kazi za kikundi hicho ni kuwahamasisha Watanzania wajivunie
utamaduni wao na washiriki kikamilifu kuufufua, kuukuza na kuulinda. Makazi ya
Kikundi yalikuwa Shariff Shamba- Ilala, Dar es Salaam, mahali zilipo ofisi za
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Dk Herbert Makoye katika mahojiano
maalumu na anasema wamejipanga kuhakikisha Taasisi hiyo inakuwa kituo cha
mafunzo ya Sanaa na Utamaduni chenye ubora uliotukuka Afrika.
Bango la TaSUBa |
|
|
Hivyo ndivyo unaweza kusema kuhusu TaSUBa. Umaarufu wake
umekwenda mbali zaidi kwa kutoa manguli katika Sanaa ambao wamesambaa duniani
kufanya kazi hizo.
Watumiaji dawa za kulevya bado tatizo Tanzania
Jamii
imetakiwa kuendelea kuwaelimisha vijana kuhusu matumizi na athari za dawa za
kulevya ili kuwaokoa vijana na kutumbukia katika kadhia hiyo hatarishi.
Akizungumza
katika Warsha ya Siku Moja kwenye Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linaloendelea
katika viunga vya TaSUBa; Eusebius Lekewe, Mshauri Nasaha wa Kituo cha
Kurekebisha Tabia za Waathirika wa Dawa za Kulevya cha Life and Hope
Rehabilitation Bagamoyo mkoani Pwani amesema tatizo linazidi kukua siku baada
ya siku hali ambayo inatishia maendeleo ya taifa.
Lekewe
amesema vijana ndio nguvu kazi ya taifa, endapo juhudi za makusudi
zisipochukuliwa maendeleo itakuwa ni ndoto kwani nguvu kazi itakuwa imepotea.
Aidha ametoa
wito kwa mashirika mbalimbali, dini, serikali na kila mmoja kuunganisha nguvu
kwani kwa tangu kituo hicho kianze wamepokea waraibu 600 ambapo 570 ni wa kiume
na 30 ni wa kike hali ambayo ameiita kuwa ni janga la kitaifa.
Hata hivyo
Lekewe amesisitiza kuwa jamii inapaswa kupiga vita michezo ya kubashiri kwani
imegeuka kuwa uraibu kwa vijana hali ambayo imekuwa ikiwasababishia madhara
zaidi ikiwamo ulevi, wizi na ngono zisizo salama.
Tamasha la
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linatia nanga Oktoba 27 mwaka huu.
TaSUBa ni kufupisho cha maneno haya 'Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo'. |
Washiriki wa warsha kuhusu matumizi ya dawa za kulevya na athari zake kwenye Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo katika Jukwaa ya Mwembeni, TaSUBa. |
Washiriki wa warsha kuhusu matumizi ya dawa za kulevya na athari zake wakifuatilia kwa makini iliyofanyika katika Jukwaa ya Mwembeni, TaSUBa, Oktoba 24, 2018 |
Washiriki wa warsha kuhusu matumizi ya dawa za kulevya na athari zake wakifuatilia kwa makini iliyofanyika katika Jukwaa ya Mwembeni, TaSUBa, Oktoba 24, 2018 |