Mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo lilianguka na baadaye kulipuka baada ya mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi.
Tukio hilo limetokea Alhamisi Juni 28, 2018 katika barabara ya Lagos - Ibadan ambayo ni miongoni mwa njia kubwa za magari jijini humo.
Wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini humo wamekaririwa wakisema milipuko inayotokana na mafuta sio kitu cha kushangaza katika taifa hilo kubwa barani Afrika kwa uzalishaji wa mafuta.
Petrol imekuwa ikisafirishwa katika mfumo mbaya nchini humo kutokana na ubovu wa barabara na vyombo vya usafirishaji.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa pole kwa tukio lililotokea. Msemaji wa Serikali Kehinde Bamigbetan ameongeza kuwa ni lazima zitafutwe njia za kuthibiti malori hayo na madereva ambao watawajibika.