![]() |
Ron Davis akihojiwa na mwandishi wa habari Jabir Johnson Novemba 2018 Mkuza, Kibaha mkoani Pwani. |
Tuesday, December 18, 2018
RON W. DAVIS: Namna alivyokuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Riadha Tanzania-3
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Makala yaliyopita tulijikita
kuangazia maisha ya awali ya mwanariadha na mwanamapinduzi katika mchezo huo
Ron William Davis na namna alivyopata nafasi ya kuzuru bara la Afrika.
Aidha katika tuliangazia
namna alivyokutana na mpiganaji wa taifa la Afrika Kusini Nelson Mandela
mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambaye alitumia mchezo wa riadha kuomba radhi wanamichezo
wa Afrika Kusini ambao walifungiwa kushiriki michuano tangu mwaka 1960 kutokana
na vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Tuliona Mandela alipopaza
sauti yake kwa watu wa Afrika ya Kusini walimwelewa na ikawa sababu mojawapo
iliyomfanya akalie kiti cha urais wa taifa hilo mwaka 1994 ikiwa ni miaka
michache baada ya kutoka jela la Rhode Island alikodumu kwa miaka 27.
Katika makala haya
tutaangazia namna alivyotua Tanzania na kuwa kocha mkuu wa timu ya riadha ya
taifa. Kwa ufupi Ron Davis ndiye kocha wa kwanza kuiletea Tanzania medali pale
alipomsimamia mkongwe Filbert Bayi na Suleiman Nyambui katika mashindano ya
kimataifa.
MICHUANO YA JUMUIYA YA
MADOLA 1978
Mwaka 1978 michuano ya
Jumuiya ya Madola ilifanyika mjini Edmonton, Alberta nchini Canada. Nigeria
iliamua kuwa haitashiriki michuano hiyo kwani ilikuwa imetoka kwenye michuano
ya All Africa Games ambayo Ron Davis alikuwa kocha huko.
Sababu kubwa ya Nigeria ya
kutoshiriki ilikuwa wazi kabisa kwa ilikuwa imegomea kuunga mkono michuano hiyo
kutokana na New Zealand kushiriki mashindano ya michezo na taifa la Afrika
Kusini wakati huo ubaguzi wa rangi ulikuwa wa kiwango cha juu.
Kitendo hicho cha Nigeria
kufanya hivyo hakikuwa kigeni kwani mwaka 1972 iliongoza mgomo wa michuano ya
Olimpiki ilifanyika mjini Munich nchini Ujerumani pia ilifanya hivyo katika
Michuano ya Olimpiki ya mwaka 1976 iliyofanyika Montreal nchini Canada.
Katika mahojiano na Ron
Davis anasema, “Nigeria ilikuwa na msimamo wa kuunga mkono mapambano dhidi ya
ubaguzi wa rangi ambao ulikuwa ukienea kwa kasi, na juhudi hizo zilienea
duniano kote.” Ron Davis analikumbuka vema tukio hilo la michuano ya Jumuiya ya
Madola kwani taifa la Canada ambao walikuwa wenyeji wa mashindano hayo
walipeleka ndege yao Air Canada nchini Algeria ambayo ilitumika kuchukua
wanamichezo wa Afrika ambao walikwenda kushiriki.
Kocha huyo anasema, “Mimi,
Lee Evans na John Carlos hatukupanda ndege hiyo na timu lakini tulitumia ndege
ya Ujerumani kwa ufadhili wa kampuni ya Puma, kwani Carlos alikuwa
akiiwakilisha Puma katika michuano ya Jumuiya ya Madola.”
Ron Davis anasema kuwa uwepo
wa Carlos uliwafaidisha kwani baada ya siku kadhaa za kuwapo mjini
Herzogenaurach miongoni mwa vitongoji mahiri katika jimbo la Bavaria nchini
Ujerumani yeye na Carlos walikwenda Edmonton wakati Lee aliitwa California.
Akiwa kwenye ndege Ron Davis
anasema alikuwa haamini kama anakwenda kwenye michuano hiyo akiwa kama kocha na
alitabasamu tu akikumbuka miaka ya nyuma ilivyokuwa katika kufikia ndoto zake.
Canada haikuwa mara yake ya kwanza lakini safari ya kutinga katika michuano
hiyo kama miongoni mwa makocha wakubwa duniani ndiyo ilimfanya atabasamu ndani
ya ndege.
Wakati naandika makala haya
nikakumbuka nukuu ya mwanamitindo na mwigizaji wa kike wa Marekani Christie
Brinkley aliposema, “Ishirikishe dunia na tabasamu lako. Ni alama ya mahusiano
mazuri (urafiki) na amani.”
Hakika hata sasa ukimuona
Ron Davis tabasamu lake bado analo hiyo ikimaanisha ndiye yule aliyetabasamu
ndani ya ndege ikimaanisha ni mtu wa amani. Na amani yake ndiyo ilimfanye
akutane na ujumbe kutoka Tanzania katika michuano hiyo.
HATUA MOJA MBELE
Aidha Ron Davis alikuwa
hajui kwa wakati huo alipokutana na kocha wa Filbert Bayi kama ingetengeneza
njia. Wakati huo kocha Sulus alikuwa akimnoa Bayi. Baada ya mazungumzo ya muda
Sulus alimtambuliza kwa Waziri wa Michezo na Utamaduni wa Tanzania alikuwapo
Edmonton.
Hapo ndipo walipopanga muda
mzuri wa kukutana ili kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu mchezo wa riadha.
Ron Davis anasema alishtushwa na namna mwakilishi huyo wa nchi alivyomkaribisha
kutokana na kwamba alikuwa bado ni kocha wa timu ya taifa ya Nigeria ingeleta
mkanganyiko lakini alisubiri nini kitakachotokea.
Unafikiri nini kilifuata
baada ya Ron Davis kukutana Kocha Sulus na Waziri wa Michezo na Utamaduni
katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mwaka 1978? Tukutane juma lijalo katika
mwendelezo wa makala haya.
Makala haya yametayarishwa
na Jabir Johnson ambaye alipata fursa ya kuzungumza na Ron Davis katika
masuala mbalimbali ya maisha yake na medani ya riadha alipotua nchini Tanzania. Pia yalichapishwa katika Gazeti la Tanzania Daima. Kwa maoni ushauri barua pepe: jaizmela2010@gmail.com
Wednesday, December 12, 2018
Lucas Moura aipeleka Spurs hatua ya 16 Ligi ya Mabingwa Ulaya
![]() |
Lucas Moura akipongezwa na wenzake baada ya kuisawazishia Tottenham |
![]() |
Lucas Moura hawakuweza kuuzuia mkwaju ulipa Spurs kusonga mbele |
![]() |
Dakika ya 85 ya mchezo ubao wa matokeo Camp Nou ulibadilika baada ya Mbrazil Lucas Moura kuisawazishia Spurs |
![]() |
Heung Min Son litoa mchango wa bao hilo akimpita Thomas Vermalen katika mchezo huo. |
![]() |
Qusmane Dembele aliwashika kweli kweli Spurs ambapo dakika ya saba ya mchezo alipachika wavuni bao la kuongoza |
![]() |
Lionel Messi aliingia akitokea mechi akichukua nafasi ya Munir El Hadadi |
Tuesday, December 11, 2018
Daei: Iran inaweza kukutana na Japan mataifa ya Asia 2019
![]() |
Ali Daei |
DEC. 11, 2018 - Mkongwe wa
kandanda nchini Iran Alli Daei amesema taifa lake linaweza kukutana katika
fainali na Japan katika michuano ya Mataifa ya Asia yanayotarajiwa kuanza
Januari 5 kwenye ardhi ya Falme za Kiarabu.
Daei anasema Japan ilionyesha mpira
mkubwa katika Kombe la Dunia nchini Russia sawa na Iran. Hata hivyo nyota huyo
anayeongoza kwa ufungaji wa mabao wa mashindano hayo akifunga mabao 14 katika
mara tatu alizoshiriki akiwa na Iran amewataja nyota wa kikosi cha kocha Melli,
Alireza Jahanbakhsh, Saman Ghoddos, Mehdi Taremi na Sardar Azmoun kuwa ni
muhimu katika kuipeleka Iran fainali za michuano hiyo hapo mwakani.
Iran ni
mabingwa mara tatu wa Kombe la Mataifa ya Asia kwa mara ya mwisho ilitwaa taji
hilo mwaka 1976.
Sunday, December 9, 2018
Uhuru wa Tanganyika 1961
![]() |
Ramani ya Tanganyika, wakati wa Utawala wa Ujerumani; Tanganyika ilikuwa ikiitwa German East Africa (GEACO) |
Taifa la Tanganyika lilijipatia uhuru wake Desemba 9, 1961
kutoka kwenye makucha ya Uingereza. Historia yake inaanzia mbali, harakati za
kudai uhuru wa Tanganyika ambayo baadaye (1964) ilikuja kuungana na Zanzibar
kuunda inayoitwa sasa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwandishi wa harakati za uhuru wa Tanganyika Mohammed Said
katika kitabu chake cha “The Life and Times of Abdulwahiid Sykes,” anasema Julius Kambarage Nyerere alikuja Dar es Salaam
mwaka 1952 akiwa kama mwalimu wa shule ya St. Francis College, Pugu.
Nyerere alikuwa na Mwapachu huko Tabora katika mwaka 1945, na
Makerere College na baadaye nchini Uingereza wakichukua masomo ya juu.
Inawezekana kwamba Nyerere kufuatia harakati za chama cha
TAA, alisikia kuhusu Abdulwahid kupitia kwa Mwapachu alipokuwa bado yuko
Uingereza. Mwapachu na Nyerere walikuwa wanafunzi katika Chuo cha Makerere wakati
ambapo Kasella Bantu na Nyerere walifundisha katika shule moja, St. Mary's
School huko Tabora.
Uhuru wa Tanganyika huwezi kuuzungumzia bila kumzungumzia
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere namna alivyopita hadi kufikia kushika madaraka
makubwa ya kuliongoza taifa.
Nyerere alipata kusema kwamba, ilikuwa dhahiri yake
kufundisha kwa muda kisha aingie kwenye siasa. Hatimaye Nyerere alifanywa
kuukubali ule uongozi ambao Tanganyika Africans Association (TAA) ilimpa.
Shindano baina ya aliyekuwa rais, Abdulwahid na Mwalimu wa
shule asiyefahamika, Julius Nyerere, lilifanyika kwenye Ukumbi wa Arnatouglo Aprili
17, 1953. Ukumbi huu ukienda ofisi ndogo za Chama chsa Mapinduzi mtaa wa
Lumumba jijini Dar es Salaam utaonyeshwa tu.
Nje ya duara la uongozi wa TAA ambao ulimpendekeza kugombea,
Nyerere alikuwa mgeni kabisa kwa wote waliokuwa na haki ya kupiga kura.
Shughuli za kisiasa za Nyerere zilianza tangu siku hii. Hapa
alikuwepo Nyerere, mgeni na mtu aliyekuwa hana historia ya kuongoza mapambano
ya watu dhidi ya serkali ya kikoloni.
Familia ya Sykes ilikuwa imehusika na siasa za kienyeji mjini
Dar es Salaam kwa takribani robo ya karne wakianzisha na kuongoza vyote viwili
vyama vya African Association na Al Jamiatul Islamiyya.
Abdulwahid kama mtoto wa Kleist Sykes alikuwa mmoja wa
familia iliyojadili hadharani masuala ya kisiasa ya siku zile na kuyaandika
wakati mwingine wakiandikiana barua na mamlaka ya kikoloni.
Uchaguzi ulikuwa wa kuinua mikono. Phombeah aliyekuwa
mfawidhi wa Ukumbi wa Arnatouglo alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo. Phombeah
aliwaomba wote wawili Abdulwahid na Nyerere kutoka nje ya ukumbi ili uchaguzi
uanze.
Wiki nzima kabla ya uchaguzi Phombeah alikuwa akizunguuka
huku na kule akimfanyia kampeni Nyerere. Lakini hakukuwa na haja ya kufanya
hivyo, duara la ndani kabisa la TAA la Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz na Rupia
lilikuwa tayari limekwishaamua kumfanya Nyerere awe rais wa chama.
Uchaguzi ilikuwa kutimiza utaratibu tu. Baada ya Abdulwahid
na Nyerere kutoka nje upigaji kura ulianza Abdulwahid "alishindwa"
uchaguzi huo ikiwa ni mara yake ya kwanza katika maisha yake yote ya siasa.
Nyerere alishinda uchaguzi huo dhidi ya Abdulwahid aliyekuwa
rais wakati huo kwa kura chache sana. Huu ulikuwa ndio mwanzo na mwisho kwa
ushawishi wa familia ya Sykes katika chama cha TAA na mwanzo wa shughuli za
kisiasa za Nyerere. Tangu siku ile historia ya kisiasa ya Tanganyika kamwe haikuwa
ile ile tena.
Dossa Aziz alikuja kutoa taarifa kwamba Abdulwahid hakushindwa
katika uchaguzi ule,
"Hakukuwa na namna yoyote Nyerere angeweza kumshinda
Abdulwahid katika Dar es Salaam ya miaka ya 1950. Abdulwahid hakushindwa katika
uchaguzi ule. Sisi sote tulitaka iwe vile. Uongozi wa TAA tulimtaka Nyerere."
Abdulwahid alikuwa mwenye kuonekana mara kwa mara, kama rais
wa TAA aliifanya ofisi yake ipendeze. Alizoea kuwakaribisha watendaji wa TAA
nyumbani kwake kwa chakula cha mchana na usiku na hili liliongeza umaarufu
wake. Wakati huo wengi walidhani Nyerere asingefaa katika nafasi ile ya
Abdulwahid.
Marehemu Tewa Said alipata kueleza kwamba siku ile kabla ya
uchaguzi pale katika Ukumbi wa Arnatouglo, Abdulwahid alikwenda nyumbani kwake
jioni.
Wakati huo Tewa alikuwa akikaa mtaa wa Pemba si mbali sana
toka nyumbani kwa Abdulwahid. Abdulwahid alimwambia Tewa haya kuhusu mabadiliko
ya uongozi ambayo waliamua yafanyike kwenye chama cha TAA;
"Tewa, kesho tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka
ya kuendesha nchi hii. Kuanzia hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna
namna ya kumnyang'anya mamlaka hayo. Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini
kila kitu kitakwenda vizuri."
Tewa akikumbuka matukio yaliyopelekea Nyerere kuchaguliwa
kama rais wa TAA alisema; "Kitu pekee alichokuwa nacho Nyerere zaidi ya Abdulwahid
kilikuwa ile digrii ya chuo kikuu. Abdulwahid kwa takribani miaka minne tangu
akamate ofisi katika mwaka 1950, alikataa kuitisha mkutano wa wajumbe kwa
sababu moja au nyingine, mpaka alipokutana na Nyerere. Ninaamini kama
Abdulwahid angekwenda Makerere tungeunda chama cha TANU mapema zaidi, labda
kabla ya mwaka 1954 na Abdulwahid angekuwa rais, hata kama angeshindana na
Nyerere."
Haya ni miongoni mwa mambo yaliyokuwapo nyuma ya uhuru wa
Tanganyika ambayo mwaka 1919 sehemu kubwa ya koloni la Kijerumani ilikabidhiwa
rasmi mikononi mwa Uingereza kama eneo la kudhaminiwa chini ya mamlaka ya
Shirikisho la Mataifa kulingana na kifungo 22 cha mkataba wa Versailles.
Wajerumani walianza kushirikia eneo la Tanganyika tangu mwaka 1886 ikiwa ni
miaka miwili baada ya Mkutano wa Berlin mwaka 1884.
![]() |
Ramani ya Afrika |