Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Thursday, September 12, 2024

Mlima Kilimanjaro, Pride of Tanzania and Africa

 

Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika, pia ni wa pili kwa urefu Duniani. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi kuliko mlima tu ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima. 

Mlima huu ambao ni mrefu kuliko yote katika Bara la Afrika na wenye barafu katika kilelele chake ingawa, upo kwenye eneo la joto karibu na Mstari wa Ikweta. Mathalani, Kibo ina theluji na barafu  kadhaa ndogo.

Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko takriban mnamo mwaka 1730.
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru Peak. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller mnamo tarehe 6 Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kijer.:Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Lori lililopinduka Sokoni Maimoria latolewa mtaroni, kazi ya kulitoa yachukua saa 4

Kazi ya kulitoa lori lililopinduka mnamo Septemba 9, 2024 ikimalizika, siku tatu baadaye majira ya saa 5:46 usiku, pembezoni mwa Soko la Maimoria  mjini Moshi. (Picha zote na JAIZMELA)


Hatimaye lori la Kenya lililopinduka Soweto mjini Moshi, karibu na Soko maarufu la Maimoria limenyanyuliwa kutoka mtaroni  mnamo Septemba 11, 2024.

Lori hilo lenye namba za usajili KBJ 139 F na trela lenye namba na usajili ZD 9542 lilipinduka za 7:30 usiku wa kuamkia mnamo Septemba 9, 2024 wakati dereva wa lori hilo alipotaka kukunja kona baada ya kukutana na kibao kilichokuwa kikimtaka asiendelee na safari.

Zoezi la kulitoa lori hilo kutoka mtaroni na kusababisha huduma ya umeme kukatwa ilianza majira ya saa 1 usiku na kumalizika saa 5:46 usiku.

Winchi yenye namba za usajili T 629 EDR lilifika katika eneo hilo na kuanza shughuli ya kulitoa mtaroni ambapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Kilimanjaro lilifika na kutoa msaada ikiwamo kukata umeme katika laini iliyokuwa imeegemewa na lori hilo.

Kikosi kazi cha Tanesco kilichokuwa na gari aina ya Land Cruiser su 44318 kilisimamia zoezi hilo kuhakikisha hakuna madhara ya umeme yanayoweza kujitokeza katika eneo la tukio.

Hata hivyo mashuhuda wa tukio hilo wametoa rai kwa madereva kuwa makini na uendeshaji wa vyombo vyao vya usafiri ili kupeusha madhara yanayojitokeza pindi ajali kama hizo zinapotokea.

Mwenyekiti wa Kituo cha Bodaboda eneo la Soko la Maimoria Jamal Hussein maarufu ‘Chawaaa’ alisema makossa yalianza kwa watengenezaji wa barabara Hari Singh & Sons ambao waliweka kibao cha kubadili uelekeo (Diversion) bila kutoa tahadhari kwanza kwani njia hiyo imekuwa ikitumiwa na malori.



Askofu Sendoro kuzikwa Septemba 17, 2024

Askofu Chediel Elinaza Sendoro
(Mei 1,1970-Septemba 9, 2024)

Halmashauri Kuu ya Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imesema mazishi ya aliyekuwa Askofu  wa (KKKT) Jimbo la Mwanga Chediel Elinaza Sendoro, yatafanyika Septemba 17 mwaka huu Wilayani humo.

Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Mathias Msemo, aliyasema hayo jana, baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha halmashauri hiyo, kilichofanyika Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, kujadili juu ya msiba huo.

“Halmashauri Kuu ya Dayosisi ya Mwanga ilikutana kwa dharura Septemba 10 majira ya asubuhi na kupanga tarehe ya maziko ya aliyekuwa Askofu Chediel Elinaza Sendoro, kuwa yatafanyika Septemba 17, Jumanne ijayo; tumeweka muda wa wiki moja kwa sababu msiba huu sio wa dayosisi pekee yake, ni msiba wa Kanisa kwa ujumla”, alisema Katibu Msemo.

Msemo alisema kuwa kwa sasa vikao mbalimbali vya Kanisa vinakaa ili kuandaa mazishi ya askofu huyo wa Kwanza wa Dayosisi hiyo.

Alisema muda huo utatoa nafasi kwa Maaaskofu wenzake, Waamini na watu wengine kupata muda mzuri wa kujitayarisha kwa mazishi hayo.

“Kifo cha Hayati Askofu Chediel Elinaza Sendoro, kimekuja wakati ambao dayosisi hiyo ilikuwa kwenye maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Dayosisi, hivyo tumekuwa kwenye taharuki kuubwa na tunawasihi waumini wa Kanisa kuwa watulivu wakati huu wa msiba.”alisema.

Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Askofu huyo ambaye alisema alikuwa ni mtu wake wa karibu ikiwemo enzi zao  wakiwa shuleni.

“Nimeupokea msiba huu kwa masikitiko makubwa sana, kwa sababu, ukiacha tu kwamba alikuwa kiongozi wangu wa kiroho pia alikuwa rafiki ambaye tulikuwa naye pamoja wakati tukisoma shule ya Sekondari ya Lutheran Junior Seminary iliyoko mkoani Morogoro na baada ya kumaliza masomo yetu yeye akaenda kwenye kazi za kiroho na mimi nikaenda kusomea maswala ya Sheria,”

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro (SACP), ajali hiyo ilitokea eneo la Kisangiro Wilayani humo.

Alisema Askofu Sendoro alikuwa akitokea Barabara ya Njiapanda ya Himo ambako gari alilokuwa akiendesha lipata ajali ya kugongana uso kwa uso na lori na hivyo kusababisha kifo chake.

Alizaliwa Mei Mosi, 1970 akiwa mtoto wa kwanza wa Askofu Elinaza Sendoro aliyewahi kuwa askofu mkuu wa dayosisi ya Mashariki na Pwani,

Baba Askofu Sendoro ameacha mjane, watoto wawili na wajukuu wawili. Askofu Chediel Sendoro  alifariki dunia Septemba 9, 2024 kwa ajili ya gari wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.


Tuesday, September 10, 2024

Maandalizi maziko ya Askofu Chediel Sendoro yanaendelea

Askofu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chediel Sendoro 

Maandalizi kwa ajili ya kumzika Askofu wa Askofu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chediel Sendoro aliyefariki dunia kwa ajali usiku wa kuamkia Jumatatu ya Septemba 9, 2024

Ajali hiyo ilitokea eneo la Kisangiro, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimaniaro, baada ya gari alilokuwa akiendesha Askofu Sendoro kugongana uso kwa uso la lori.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alikaririwa na Mwananchi kuwa ajali hiyo ilitokea leo saa 1:30 usiku, wakati gari lililokuwa likiendeshwa na Askofu huyo kutokea barabara ya Njiapanda ya Himo-Mwanga kuyapita magari mengine na kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania   lililokuwa likitokea Tanga -Arusha.