Sunday, June 16, 2024

Zuberi Cup Tournament 2024; ni Shiiida! Yaanza kwa Kishindo

Zuberi Cup Tournament 2024: Shaffih Dauda, Mgeni rasmi wa ufunguzi wa Mashindano ya Soka maarufu katika Mkoa wa Kilimanjaro  Zuberi Cup Tournament akionyesha jezi aliyopewa na Mwasisi wa Mashindano hayo ya soka Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Injinia Zuberi Abdallah Kidumo (kulia), na kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Chama cha Soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Thabit Kombo. Ufunguzi huo umefanyika mnamo Juni 16, 2024 kwa mechi ya kwanza baina ya mabingwa watetezi Pasua Big Stars na Wazalendo. (Picha na. JAIZMELA/Jabir Johnson, Moshi) 


Michuano maarufu ya soka katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro Zuberi Cup Tournament mwaka huu imeanza kwa kishindo kulishuhudiwa Mabingwa Watetezi Pasua Big Stars wakipepetana na Wazalendo katika mchezo wa ufunguzi.


Michuano hiyo iliyopewa jina la Zuberi Cup Tournament kwa heshima ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Abdallah Kidumo inazikutanisha timu 25 msimu huu katika kutafuta bingwa kwa siku 30.

Katika ufunguzi wake Zuberi Cup Tournament 2024 imeshuhudiwa Uwepo wa Mwasisi wa Mashindano ya Mpira katika hatua ya mitaaa hapa nchini maarufu Ndondo Cup Shaffih Dauda.

Dauda katika ujumbe wake kwa mashabiki na wadau wa soka nchini amewataka kuungana ili kuyafanya Mashindano hayo ya mitaa hapa nchini kuwa na hadhi

Aidha amewataka Shirikisho la Soka la Tanzania TFF kuanza Sasa kutazama suala la Viwanja vya nyasi bandia katika Mitaa kwani Watanzania hawakuzaliwa wacheze katika Viwanja vibovu.

Wake, waume na watoto wameshuhudia ufunguzi huo wa nguvu ambao umedhihirisha soka ni mchezo unaopendwa na wengi hapa ulimwenguni.

Maisha ya kila siku ya wapenzi wa soka katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro yamekuwa desturi ya kuionyesha katika Zuberi Cup Tournament 2024. Burudani mbalimbali akiwamo Asha Ngedere wa Njoro kupamba ufunguzi huo.

Awali Mwenyekiti wa Mashindano hayo mwaka huu Mwàlimu Japhet Mapande amezitakia timu kujizuia kufanya vurugu na mashabiki wao.

Mwakilishi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro KRFA Thabit amewataka wadau wa soka kuacha kurudishana nyuma pindi Jambo zuri la kimpira linapofanywa.































0 Comments:

Post a Comment