Mwasisi wa Mashindano ya soka mjini Moshi Zuberi Cup Tournament; Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Kidumo
Mashindano ya soka kila mwishoni mwa msimu mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ya Zuberi Cup yamezinduliwa rasmi mnamo Mei 18, 2024 kwa kikao cha kwanza timu washiriki.
Mbunge wa Moshi Mjini Priscus Tarimo amezindua rasmi Zuberi Cup Tournament akiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Kilimanjaro Isaac Gaga na mwanzilishi wa Mashindano hayo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Kidumo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Injinia Zuberi Kidumo amezitakia kila la Kheri timu shiriki katika maandalizi huku akisisitiza kuwa nidhamu na kuifanya mchezo wa soka kuishi katika hadhi yake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema msimu huu michuano hiyo imekuja kipekee hususani katika suala la zawadi huku wakitaka hadhi ya Zuberi Cup Tournament ibakie katika kata ya Njoro isihamishwe.
Awali uzinduzi huo ulianza kwa maombi yaliyofanywa na Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwà limu Japhet Mapande.
Pia Mwenyekiti wa Soka mkoa Kilimanjaro Munisi amesema wanajivunia mafanikio makubwa ya timu za mkoa wa Kilimanjaro licha ya kushindwa kuendelea mbele.
Msimu huu mshindi ataondoka na Kombe na fedha taslimu shilingi milioni tatu, mshindi wa pili atachukua shilingi milioni mbili na mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.
Bingwa wa msimu wa 2023 ni klabu ya Pasua Big Stars. Kinachofuata ni vikao vya timu washiriki namna ya kuanza michuano hiyo.
0 Comments:
Post a Comment