Diwani wa Kata ya Korongoni Heavenlight Kiyondo |
Diwani wa Kata ya Korongoni, Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro HeavenLight Kiondo, amesema kuwa mikopo ya asilimia 10% inayotarajiwa kutolewa na Serikali itasaidia Wanawake Wajasiriamali, Vijana na Watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi.
Kiyondo amesema hayo Mei 20, 2024 wakati akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata yake na kuzitafutia ufumbuzi.
Amesema urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10% ambayo hutolewa na Serikali kupitia Halmashauri bila riba, itawasaidia wanawake Wajasiriamali, Vijana na wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kwa kubuni fursa mbalimbali za kiuchumi, huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikopo hiyo kurejeshwa tena baada ya kusitishwa.
Naye Mkazi wa Kata ya Korongoni Ruth Joseph, mikopo iliyokuwa ikitolewa na halmashauri ilitusaidia kujikwamu kwenye mambo mbalimbali zikiwemo biashaea zetu, kwani aniliweza kuongeza mtaji kwenye biashara yangu.
Aidha amesema kusitishwa kwa mikopo hiyo kutolewa, ilipelekea watu wengi kukimbilia kwenye mikopo yenye riba kubwa (Kauha damu) na hivyo kujikuta wakishindwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati jambo ambalo lilipelekea baadhi yao wakiuziwa mali zao huku wengine kupoteza maisha.
Mkazi mwingine wa Kata hiyo Regina Oscar amesema mkopo wa Halmashauri ulimsaidia kupanua biashara yake na hivyo kumnyanyua kimaisha
Wakazi wa Kata ya Korongoni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wamemshukuru diwani huyo kwa ziara yake ya mtaa kwa mtaa, ambayo ameianzisha kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi katika mitaa yao ili kuzipatia changamoto hizo ufumbuzi wa akudumu.
0 Comments:
Post a Comment