Hospitali Maalum ya Afya ya Jamii na Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto Maalum (KIDH) imefungua ukurasa mpya kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu Sugu hususani watoto kuanza kulazwa Hospitalini hapo wakiwa na Wazazi wao bila malipo yoyote.
Wakitoa shuhuda zao hivi karibuni katika ziara ya siku moja katika Hifadhi ya Taifa Tarangire mkoani Manyara kwa wagonjwa wa Kifua Sugu wanaoendelea kupewa dawa katika Hospitali ya Kibong'oto wamesema wakati wanaingia hapo hali zao zilikuwa mbaya kiasi cha kupoteza matumaini ya kuishi.
Ushuhuda wa mama huyu mwenye watoto saba mzaliwa wa Kibondo mkoa wa Kigoma unadhihirisha wazi namna Hospitali Maalum ya Afya ya Jamii na Magonjwa Ambukizi Kibong'oto inavyojitahidi kwa kila hali kuhakikisha Kifua Kikuu Sugu kinatokomezwa kwa watu wazima na watoto.
Akizungumza kuhusu ziara hiyo muuguzi wa Hospitali hiyo Sara Mtoi amesema kuna haja ya kuendelea kujitolea zaidi kuwasaidia wenye changamoto ya Kifua Kikuu sugu kwa kila hali.
Aidha Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali Maalum ya Afya ya Jamii na Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto WazoEli Mshana amesema uboreshaji wa Huduma umekuwa msingi mkubwa wa wagonjwa wa Kifua Kikuu Sugu kupona wakitokea hospitalini hapo.
Wazoeli amesisitiza ulazima wa Jamii kushirikiana kwa pamoja pindi wanapowaona wenye dalili za Kifua Kikuu Sugu kupelekwa haraka kwa ajili ya kuanza matibabu ili Kuzuia kuenea kwa maradhi hayo.
Kwa upande wake Muongoza Watalii Hifadhi ya Taifa Tarangire Anthony Andrea, ameushukuru uongozi wa Kibong'oto kwa kuweka utaratibu wa kuwa wanawaleta wagonjwa wa Kifua Kikuu Sugu waliopona kuchagua kutembelea hifadhi hiyo.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania kutembelea vivutio vya Utalii ili kujifunza namna ya kujitegemea hatua ambayo inakuza maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake Mratibu Mpya wa LHL International Veronica Alavarez ameweka bayana adhma yake ya kupunguza mzigo kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu Sugu wanaohudumiwa Hospitali ya Kibong'oto akianza pale walipoishia watangulizi waliopita
0 Comments:
Post a Comment