Imeelezwa kuwa matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni yanatajwa kuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili, ambayo yanapelekea baadhi ya wanafunzi kujikuta wakiingia katika kutazama picha za utupu, na hivyo kuwasababishia athari za kisaikolojia na hivyo kuwasababishia kuacha kufikiria kusoma na kufanya mambo ambayo hayako kimaadili.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Olmorok Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro Inspecter Msike Francis Banda, wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mpirani iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani humo, kuhusiana na matukio ambayo yamekuwa yakiikabili jamii ikiwemo masuala ya mimba mashuleni.
Amesema matumizi ya simu kwa wanafunzi shuleni, yamekuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili kwao, yanaweza kudhibitiwa endapo wamiliki wa shule, walimu na wazazi watasimamia sheria zitakazosaidia kuwabana wanafunzi kumiliki simu.
Amesema wao kama wasimamizi wa sheria ameona kutumia hadhara hiyo kutoa elimu kwa jamii, kuhusiana na mimba mashuleni, matumizi ya dawa za kulevya, matumizi ya simu kwa wanafunzi ambayo yanapelekea wanafunzi kujikuta wanaingia katika kutazama video za utupu zinazowaletea adhari ya kisaikolojia.
Aidha amesema vitendo vya ukatili, ushoga na ubakaji vimekuwa ni tatizo kubwa nchini Tanzania na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili hatua za kisheria ziweze kuchujkuliwa dhidi ya watu ambao wanahusika na vitendo hivyo.
Kwa upande wake Mwalimu mstaafu wa shule ya Ufundi Moshi Japhet Mpande amesema wanafunzi wanapokuwa na simu shule hawezi kukaa na kujali masomo yao, bali muda mwingi watakuwa wakichati na simu na kushindwa kumsikiliza mwalimu.
Amesema pamoja na kuwa katika kipindi cha utandawazi, mawasiliano ni muhimu kwa kila mmoja, japo kuwa katika matumizi hayo kuna madhara ya matumizi ya simu kwa wanafunzi kwa vile wengi wao hutazama picha za ngono na kutumiana meseji za mapenzi wakati wa masomo.
Aidha amesema miaka ya nyuma wazazi walikuwa wakiwafundisha watoto wao namna ya kuishi na jamii, ukarimu na kwamba watotoo walilelewa kimaadili, lakini kwa sasa imekuwa tofauti, jirani akimkuta mtoto anafanya jambo baya akimchapa anakwenda kushitakiwa.
Naye mmoja wa wanafunzi waliosoma shule ya Ufundi Moshi Rodrick Mmari, amesema kuwa simu huleta madhara kwa wanafunzi kwa vile ni chanzo cha kufeli mitihani yao kwani baadhi yao hutumia muda wa kujisomea kwa kuongea na simu na wapenzi wao.
0 Comments:
Post a Comment