Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Monday, May 20, 2024

Urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10% kusaidia Wajasiriamali kiuchumi

Diwani wa Kata ya Korongoni Heavenlight Kiyondo


Diwani wa Kata ya Korongoni, Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro  HeavenLight Kiondo, amesema kuwa mikopo ya asilimia 10% inayotarajiwa kutolewa na Serikali itasaidia Wanawake Wajasiriamali, Vijana na Watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi. 

Kiyondo amesema hayo Mei 20, 2024 wakati akizungumzia changamoto  mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata yake na kuzitafutia ufumbuzi. 

Amesema urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10% ambayo  hutolewa na Serikali kupitia Halmashauri bila riba, itawasaidia wanawake Wajasiriamali,  Vijana na wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kwa kubuni fursa mbalimbali za kiuchumi, huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikopo hiyo kurejeshwa tena baada ya kusitishwa.

 

Naye Mkazi wa Kata ya Korongoni Ruth Joseph, mikopo iliyokuwa ikitolewa na halmashauri ilitusaidia kujikwamu kwenye mambo mbalimbali zikiwemo biashaea zetu, kwani aniliweza kuongeza mtaji kwenye biashara yangu.

 

Aidha amesema kusitishwa kwa mikopo hiyo kutolewa, ilipelekea watu wengi kukimbilia kwenye mikopo yenye riba kubwa (Kauha damu) na hivyo kujikuta wakishindwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati jambo ambalo lilipelekea  baadhi yao wakiuziwa mali zao huku wengine kupoteza maisha.

 

Mkazi mwingine wa Kata hiyo Regina Oscar amesema  mkopo wa Halmashauri ulimsaidia kupanua biashara yake na hivyo  kumnyanyua kimaisha

 

Wakazi wa Kata ya Korongoni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wamemshukuru diwani huyo kwa ziara yake ya mtaa kwa mtaa, ambayo ameianzisha kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi katika mitaa yao ili kuzipatia changamoto hizo ufumbuzi wa akudumu.


ZUBERI CUP TOURNAMENT 2024: Mipira 80 yatolewa timu washiriki, Donge Nono latangazwa kwa mshindi

Mwasisi wa Mashindano ya soka mjini Moshi Zuberi Cup Tournament; Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Kidumo 

Mashindano ya soka kila mwishoni mwa msimu mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ya Zuberi Cup yamezinduliwa rasmi mnamo Mei 18, 2024 kwa kikao cha kwanza timu washiriki.


Uzinduzi huo umeenda sambamba na timu washiriki kwa ujumla kupewa mipira 80 ambapo kila timu imeondoka na mipira miwili huku timu zikisisitizwa kuwa na viongozi walio imara ili kuijenga vizuri timu zao.


Mbunge wa Moshi Mjini Priscus Tarimo amezindua rasmi Zuberi Cup Tournament akiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Kilimanjaro Isaac Gaga na mwanzilishi wa Mashindano hayo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Injinia Zuberi Kidumo.


Kwa upande wake Mstahiki Meya Injinia Zuberi Kidumo amezitakia kila la Kheri  timu shiriki katika maandalizi huku akisisitiza kuwa nidhamu na kuifanya mchezo wa soka kuishi katika hadhi yake.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema msimu huu michuano hiyo imekuja kipekee hususani katika suala la zawadi huku wakitaka hadhi ya Zuberi Cup Tournament ibakie katika kata ya Njoro isihamishwe.


Awali uzinduzi huo ulianza kwa maombi yaliyofanywa na Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwàlimu Japhet Mapande.


Pia Mwenyekiti wa Soka mkoa Kilimanjaro Munisi amesema wanajivunia mafanikio makubwa ya timu za mkoa wa Kilimanjaro licha ya kushindwa kuendelea mbele.


Msimu huu mshindi ataondoka na Kombe na fedha taslimu shilingi milioni tatu, mshindi wa pili atachukua shilingi milioni mbili na mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.


Bingwa wa msimu wa 2023 ni klabu ya  Pasua Big Stars. Kinachofuata ni vikao vya timu washiriki namna ya kuanza michuano hiyo.