Watanzania wameitaka serikali kuzipa fursa taasisi nyingine imara zinazoweza kupambana na majanga ya moto yanapotokea nchini badala ya kutegemea Jeshi la Zimamoto pekee kufanya shughuli hiyo kutokana na idadi ya watu kuongezeka kila mwaka huku vifaa vya Jeshi hilo vikishindwa kwenda na kasi ya mabadiliko.
Soko la Mbuyuni ni miongoni mwa masoko maarufu makubwa nchini ambayo yameingia katika orodha ya kuteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara, ndugu jamaa na marafiki kuathirika kisaikolojia na wengine kupoteza maisha kutokana na mshtuko.
Masoko mengine ni kama vile Soko la Mwanjelwa mkoani Mbeya, Soko la Mandela lililopo Sumbawanga mkoani Rukwa, Soko Kuu la Mpanda mkoani Katavi na Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam ambayo yamewahi kukutana na majanga ya moto.
Wakizungumza na EATV kwa nyakati tofauti wakazi wa Manispaa
ya Moshi wamesema kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu imewafungua
na kuitaka serikali kuruhusu taasisi nyingine kudhibiti majanga ya moto.
“Baada ya zimamoto kurudishwa wizara ya mambo ya ndani ndio
mambo yalipoharibika, ni vema kurirudisha lijitegemee kabisa au kuleta washindani
nje ya mfumo ikiwamo kuziruhusu taasisi nyingine kusaidia kudhibiti majnaga ya
moto,” alisema Hassan Parangadau
0 Comments:
Post a Comment