Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Thursday, December 27, 2018

Gareth Bale mfungaji bora Fifa Club World Cup 2018


FIFA Club World Cup mwaka 2018 imemalizika kukishuhudiwa Real Madrid ikiweka rekodi mpya kwa klabu hizo kutwaa ubingwa mara nne tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo.

Madrid ambao ni mabingwa wa Ulaya waliwatandika wenyeji Al Ain kwa mbao 4-1 ambao waliwashangaza wengi kwa kuitoa miamba ya Amerika Kusini River Plate katika hatua za awali. 

Rekodi nyingine zilizowekwa katika michuano hiyo mshambuliaji wa Wales na klabu ya Real Madrid Gareth Bale alichukua kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo mwaka huu kwa kufunga mabao matatu akifuatiwa na Rafael Santos Borre wa River Plate.

Msimamo baada ya michuano kumalizika
1.     Real Madrid
2.     Al Ain
3.     River Plate
4.     Kashima Antlers
5.     Esperance de Tunis
6.     CD Guadalajara
7.     Team Wellington

Viwanja vilivyotumika
  • Zayed Sports City Stadium, Abu Dhabi
  • Hazza Bin Zayed Stadium, Al Ain
Mabao yaliyofungwa
  • 33 (4.1 per game)
Wafungaji walioongoza
  • Gareth Bale (Real Madrid) - 3 goals
  • Rafael Santos Borre (River Plate) - 3 goals
  • Gonzalo Martinez (River Plate) - 2 goals
Tuzo
  • adidas Golden Ball: Gareth Bale (Real Madrid)
  • adidas Silver Ball: Caio (Al Ain)
  • adidas Bronze Ball: Rafael Santos Borre (River Plate)
  • FIFA Fair Play Award: Real Madrid

Friday, December 21, 2018

Gareth Bale anyatia kiatu cha dhahabu Fifa Club World Cup 2018


 
Gareth Bale dhidi ya Kashima Antlers katika mchezo wa Fifa Club World Cup mwaka 2018.
Mshambualiaji Gareth Bale wa Real Madrid, ameonyesha nia ya kutaka kuondoka na kiatu cha dhahabu katika mashindano ya Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia. 

Mshambuliaji huyo juzi alifunga mabao matatu 'hat-trick' na kuiwezesha timu yake kuizamisha Kashima Antlers ya Japan kwa mabao 3-1 katika mechi ya nusu fainali na sasa itacheza fainali na wenyeji Al Ain ya Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Kocha wa Real, Santiago Solari, amemfagilia Bale, ambaye amefikisha mabao sita katika mechi tano walizocheza hadi sasa, huku Real ikiwania kutwaa taji la tatu mfululizo la michuano hiyo. 

Mechi ya fainali itachezwa kesho kwenye Uwanja wa Zayed Sports City, mchezo unaoonekana kuvuta hisia za wengi ikizingatiwa Al Ain ya Abu Dhabi iliwaduwaza wengi baada ya kuing'oa kwa changamoto ya mikwaju ya penati bingwa wa Amerika ya Kusini, River Plate ya Argentina.
Kocha Santiago Solari akizungumza jambo na Gareth Bale baada ya kumaliza mchezo dhidi  ya Kashima Antlers. Bale alifunga 'hat trick'

Tuesday, December 18, 2018

RON W. DAVIS: Namna alivyokuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Riadha Tanzania-3


Ron W. Davis Novemba 2018 alikuja Tanzania kwa mara ya pili.
DAR ES SALAAM, TANZANIA
Makala yaliyopita tulijikita kuangazia maisha ya awali ya mwanariadha na mwanamapinduzi katika mchezo huo Ron William Davis na namna alivyopata nafasi ya kuzuru bara la Afrika. 

Aidha katika tuliangazia namna alivyokutana na mpiganaji wa taifa la Afrika Kusini Nelson Mandela mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambaye alitumia mchezo wa riadha kuomba radhi wanamichezo wa Afrika Kusini ambao walifungiwa kushiriki michuano tangu mwaka 1960 kutokana na vitendo vya ubaguzi wa rangi. 

Tuliona Mandela alipopaza sauti yake kwa watu wa Afrika ya Kusini walimwelewa na ikawa sababu mojawapo iliyomfanya akalie kiti cha urais wa taifa hilo mwaka 1994 ikiwa ni miaka michache baada ya kutoka jela la Rhode Island alikodumu kwa miaka 27. 

Katika makala haya tutaangazia namna alivyotua Tanzania na kuwa kocha mkuu wa timu ya riadha ya taifa. Kwa ufupi Ron Davis ndiye kocha wa kwanza kuiletea Tanzania medali pale alipomsimamia mkongwe Filbert Bayi na Suleiman Nyambui katika mashindano ya kimataifa.

MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA 1978
Mwaka 1978 michuano ya Jumuiya ya Madola ilifanyika mjini Edmonton, Alberta nchini Canada. Nigeria iliamua kuwa haitashiriki michuano hiyo kwani ilikuwa imetoka kwenye michuano ya All Africa Games ambayo Ron Davis alikuwa kocha huko. 

Sababu kubwa ya Nigeria ya kutoshiriki ilikuwa wazi kabisa kwa ilikuwa imegomea kuunga mkono michuano hiyo kutokana na New Zealand kushiriki mashindano ya michezo na taifa la Afrika Kusini wakati huo ubaguzi wa rangi ulikuwa wa kiwango cha juu. 

Kitendo hicho cha Nigeria kufanya hivyo hakikuwa kigeni kwani mwaka 1972 iliongoza mgomo wa michuano ya Olimpiki ilifanyika mjini Munich nchini Ujerumani pia ilifanya hivyo katika Michuano ya Olimpiki ya mwaka 1976 iliyofanyika Montreal nchini Canada. 

Katika mahojiano na Ron Davis anasema, “Nigeria ilikuwa na msimamo wa kuunga mkono mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi ambao ulikuwa ukienea kwa kasi, na juhudi hizo zilienea duniano kote.” Ron Davis analikumbuka vema tukio hilo la michuano ya Jumuiya ya Madola kwani taifa la Canada ambao walikuwa wenyeji wa mashindano hayo walipeleka ndege yao Air Canada nchini Algeria ambayo ilitumika kuchukua wanamichezo wa Afrika ambao walikwenda kushiriki. 

Kocha huyo anasema, “Mimi, Lee Evans na John Carlos hatukupanda ndege hiyo na timu lakini tulitumia ndege ya Ujerumani kwa ufadhili wa kampuni ya Puma, kwani Carlos alikuwa akiiwakilisha Puma katika michuano ya Jumuiya ya Madola.” 

Ron Davis anasema kuwa uwepo wa Carlos uliwafaidisha kwani baada ya siku kadhaa za kuwapo mjini Herzogenaurach miongoni mwa vitongoji mahiri katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani yeye na Carlos walikwenda Edmonton wakati Lee aliitwa California. 

Akiwa kwenye ndege Ron Davis anasema alikuwa haamini kama anakwenda kwenye michuano hiyo akiwa kama kocha na alitabasamu tu akikumbuka miaka ya nyuma ilivyokuwa katika kufikia ndoto zake. Canada haikuwa mara yake ya kwanza lakini safari ya kutinga katika michuano hiyo kama miongoni mwa makocha wakubwa duniani ndiyo ilimfanya atabasamu ndani ya ndege. 

Wakati naandika makala haya nikakumbuka nukuu ya mwanamitindo na mwigizaji wa kike wa Marekani Christie Brinkley aliposema, “Ishirikishe dunia na tabasamu lako. Ni alama ya mahusiano mazuri (urafiki) na amani.” 

Hakika hata sasa ukimuona Ron Davis tabasamu lake bado analo hiyo ikimaanisha ndiye yule aliyetabasamu ndani ya ndege ikimaanisha ni mtu wa amani. Na amani yake ndiyo ilimfanye akutane na ujumbe kutoka Tanzania katika michuano hiyo.

HATUA MOJA MBELE
Ron Davis akihojiwa na mwandishi wa habari Jabir Johnson Novemba 2018 Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.
Ron Davis anasema, “Siku moja nikiwa katika mazoezi ya kukimbia, yoga na kujinyoosha katika njia za Chuo Kikuu cha Alberta wakati michuano hiyo ikiendelea nilienda kwa kocha wake wakati ambaye siku hiyo alikuwa na Filbert Bayi wakifanya mazoezi.” 

Aidha Ron Davis alikuwa hajui kwa wakati huo alipokutana na kocha wa Filbert Bayi kama ingetengeneza njia. Wakati huo kocha Sulus alikuwa akimnoa Bayi. Baada ya mazungumzo ya muda Sulus alimtambuliza kwa Waziri wa Michezo na Utamaduni wa Tanzania alikuwapo Edmonton. 

Hapo ndipo walipopanga muda mzuri wa kukutana ili kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu mchezo wa riadha. Ron Davis anasema alishtushwa na namna mwakilishi huyo wa nchi alivyomkaribisha kutokana na kwamba alikuwa bado ni kocha wa timu ya taifa ya Nigeria ingeleta mkanganyiko lakini alisubiri nini kitakachotokea.

Unafikiri nini kilifuata baada ya Ron Davis kukutana Kocha Sulus na Waziri wa Michezo na Utamaduni katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mwaka 1978? Tukutane juma lijalo katika mwendelezo wa makala haya.

Makala haya yametayarishwa na Jabir Johnson ambaye alipata fursa ya kuzungumza na Ron Davis  katika masuala mbalimbali ya maisha yake na medani ya riadha alipotua nchini Tanzania. Pia yalichapishwa katika Gazeti la Tanzania Daima. Kwa maoni ushauri barua pepe: jaizmela2010@gmail.com

Wednesday, December 12, 2018

Lucas Moura aipeleka Spurs hatua ya 16 Ligi ya Mabingwa Ulaya

Lucas Moura akipongezwa na wenzake baada ya kuisawazishia Tottenham
Lucas Moura hawakuweza kuuzuia mkwaju ulipa Spurs kusonga mbele
Dakika ya 85 ya mchezo ubao wa matokeo Camp Nou ulibadilika baada ya Mbrazil Lucas Moura kuisawazishia Spurs
Heung Min Son litoa mchango wa bao hilo akimpita Thomas Vermalen katika mchezo huo.
Qusmane Dembele aliwashika kweli kweli Spurs ambapo dakika ya saba ya mchezo alipachika wavuni bao la kuongoza

Lionel Messi aliingia akitokea mechi akichukua nafasi ya Munir El Hadadi