Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Monday, March 17, 2025

Godbless Lema: Wafanyabiashara wa Kichina wameleta ugumu kwa Wafanyabiashara Wazawa

 

Godbless Lema, mbunge wa zamani Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema; mnamo tarehe 21 Januari 2025 aliteuliwa rasmi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho cha upinzani nchini Tanzania; baada ya Tundu Lissu kushika nafasi ya Uenyekiti. (Picha na MAKTABA/Jaizmela)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema wafanyabiashara wazawa nchini wamedharauliwa vya kutosha kutokana na namna ambavyo serikali imewaruhusu raia wa China kushikilia sekta hiyo kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni katika kampeni ya ‘Tone Tone’  ambayo inaendeshwa na Chadema kwa madhumuni ya kukusanya fedha kidogo kidogo kutoka kwa watanzania; Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini Godbless Lema alisema wafanyabiashara wazawa, wanakutana na changamoto za upatikanaji wa mikopo na usaidizi wa kifedha, jambo ambalo linaweza kupunguza ushindani wao.

Lema aliongeza kuwa wafanyabiashara wa China wamekuwa wakiingiza bidhaa zao kwa bei nafuu ambazo zinaweza kushindana na bidhaa zinazozalishwa na wafanyabiashara wazawa, jambo ambalo limekuwa likisababisha sekta hiyo kwa wazawa kuwa dhaifu.

Katika kampeni ya Tone Tone Lema alisema wafuasi wa Chadema wanapaswa kujenga mfumo wa kukichangia chama ili kufanikisha malengo yake bila kutegemea msaada kutoka kwa serikali au vyanzo vya nje.

“Inafaa kuzingatia kwamba Michango inasaidia chama kusimamia haki za raia na kuhimiza utawala bora. Kwa mfano, Chadema, kama chama cha upinzani, kinapochangiwa fedha, kinaweza kuendesha kampeni za kuelimisha umma kuhusu haki zao, kutetea demokrasia, na kupigania mabadiliko ya kisiasa ili kuhakikisha usawa na haki kwa kila Mtanzania,” alisisitiza Mjumbe huyo wa Chadema

Viongozi wa Chadema wanaposimama na kuhamasisha michango ya Watanzania kwa chama hicho, wanatoa taswira ya chama kinachotegemea msaada wa raia ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa, hasa katika mazingira ya ukosefu wa rasilimali kutoka kwa vyanzo vya kawaida kama vile serikali au wahisani wa nje.

Chadema sio wa kwanza, Katika kipindi cha Vita vya Vietnam, chama cha Viet Minh, kilichoongoza mapambano ya uhuru dhidi ya Ufaransa na baadaye Marekani, kilitegemea michango kutoka kwa wananchi na mashirika ya kiraia ili kudumisha harakati za vita na kuhamasisha jamii.

Tundu Lissu na wenzake sio wa kwanza, kufanya kampeni hiyo; Mahatma Gandhi alikuwa kiongozi muhimu katika harakati ya uhuru ya India dhidi ya utawala wa Uingereza. Fidel Castro na chama cha Maandamano ya Julai 26 walikusanya michango kutoka kwa wananchi ili kusaidia mapambano dhidi ya utawala wa Batista.

Pia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya kupata uhuru, alihamasisha michango kutoka kwa wananchi ili kuendeleza maendeleo ya taifa na kujenga chama cha TANU;

Thomas Sankara, ambaye aliongoza mapinduzi ya Burkina Faso mwaka 1983, alihamasisha wananchi kutoa michango ili kufanikisha ajenda ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Sankara alisisitiza ushirikiano wa wananchi na akahamasisha mchango wa kifedha, mali, na rasilimali nyingine kwa ajili ya kupambana na umasikini, kupigana na rushwa, na kuboresha ustawi wa jamii.

Hivyo basi; kimataifa, viongozi wa Chadema wanapohamasisha michango, wanaweza kuonesha kwamba chama hicho kinapigania demokrasia ya kweli na utawala bora, na kuwa na msaada wa watu wa kawaida ikiwa ni ishara ya kuungwa mkono na wananchi dhidi ya mifumo ya kisiasa isiyokuwa na uwazi.

Hii pia inaweza kuvutia uangalizi kutoka kwa mashirika ya kimataifa na wadau wa demokrasia na haki za binadamu, kwani michango ya wananchi inaweza kutafsiriwa kama ishara ya ushiriki wa wananchi katika mchakato wa kisiasa, jambo linalothaminiwa kimataifa.

MWISHO

 

 

Saturday, March 8, 2025

Unywaji wa Soda watia fora wanawake Moshi DC

 

Mashindano ya unywaji wa soda, ingawa yanaonekana kuwa ya kufurahisha na ya kuburudisha, yana manufaa machache katika muktadha wa afya na ustawi. Hata hivyo, kuna baadhi ya faida zinazoweza kupatikana kutokana na mashindano haya:

  1. Burudani na furaha: Mashindano haya hutoa furaha kwa washiriki na watazamaji. Hutoa fursa ya kufurahi, kucheka, na kushindana kwa njia ya kirafiki, ambayo inaweza kuongeza hali ya furaha na umoja kati ya washiriki na jamii.

  2. Kukuza uhusiano wa kijamii: Kama michezo mingine, mashindano haya yanaweza kuleta watu pamoja. Washiriki huungana katika shindano moja na watu kutazama, na hivyo inatoa nafasi kwa jamii kushirikiana na kuimarisha uhusiano wa kijamii.

  3. Kuboresha ustadi wa kimwili: Ingawa si mchezo unaohitaji juhudi nyingi, mashindano ya unywaji wa soda yanaweza kusaidia kuboresha ustadi wa kimwili wa washiriki. Unywaji haraka wa soda unahitaji udhibiti wa mwili, pumzi, na kasi, ambayo inaweza kuhimiza ustadi wa kimwili.

  4. Kukuza roho ya ushindani: Mashindano haya yanaweza kuchochea roho ya ushindani na kujitolea kwa washiriki, kwani wanapojitahidi kushinda, wanajifunza kuhusu kushindana kwa njia ya haki na kujiamini.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba masuala ya kiafya yanapaswa kuzingatiwa. Unywaji wa soda kwa kasi kunaweza kusababisha matatizo ya kichwa, usumbufu wa tumbo, au hata kumeza hewa nyingi ambayo inaweza kusababisha maumivu ya tumbo. Kwa hiyo, ingawa kuna manufaa ya kijamii na ya furaha, ni muhimu kuwa na uwiano na kujali afya wakati wa kushiriki katika aina hii ya mashindano.







Mchezo wa Mayai unatoa Taswira gani Moshi DC


Michezo kama kukimbia na yai katika kijiko mdomoni hutoa taswira ya michezo ya kufurahisha na ya kuburudisha. Inaonekana kama mchezo wa kijamii unaolenga kushirikisha watu kwa furaha na shindano la kirafiki. Huu ni mchezo ambao hufanya washiriki kuwa na umakini wa juu na udhibiti, kwa sababu wanahitaji kuhakikisha yai lisisukume kutoka kwenye kijiko kilicho mdomoni wakati wanakimbia.

Pia, kuna taswira ya ucheshi na furaha, kwani washiriki wengi wanajikuta wakicheka au kuanguka kutokana na changamoto ya kudhibiti yai na kijiko. Huu ni mchezo unaohusisha ustadi wa kimwili, lakini pia unatoa nafasi kwa watu kutabasamu na kufurahi pamoja, jambo linaloimarisha uhusiano wa kijamii.

Mbio za Magunia kivutio Siku ya Wanawake Moshi DC 2025

 

Michezo kama hii inaweza kuonekana kama sehemu ya shughuli zinazohusiana na majukumu ya kijinsia, ambapo wanawake wanaweza kutazamwa kama wahusika wa kufanya kazi au majukumu ya familia na jamii. Hata hivyo, baadhi ya wanawake wanaweza kuona michezo ya aina hii kama njia ya kutoa ujasiri na kuwa sehemu ya sherehe au mabadiliko ya kijamii.


Wanawake Moshi DC watoana Jasho kukimbiza kuku

 

Kama michezo mingine, kukimbiza kuku kunaweza pia kuwa na ushindani na kutoa nafasi kwa wanawake kuonyesha umakini, ustadi, na ari ya kushinda. Hii inaweza kuleta taswira ya nguvu, juhudi, na kujitolea.

Mo Dewji bilionea wa 1588 duniani 2025, Tajiri pekee Orodha ya Forbes kutoka Tanzania

Kwa mujibu wa Forbes inasema tajiri namba moja nchini Tanzania Mohammed Dewji (49) maarufu Mo katika nafasi za mabilionea mwaka 2025 ni 1588.

Mo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa METL amekuwa akifanya kazi Afrika Mashariki na Kati katika nchi za Kenya, Ethiopia, Uganda na Tanzania.

Hadi tarehe 8 Machi 2025 Mo ametajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani 2.2 bilioni ikimweka katika nafasi hiyo; Utajiri huo umepanda kutoka Dola la Kimarekani 1.8 bilioni Januari 2024 ukimweka wakati huo katika nafasi ya 12 barani Afrika.

Mnamo mwaka 2016 ndiye Mfanyabiashara pekee nchini Tanzania alisaini Giving Pledge akitoa ahadi ya kujitolea walau nusu ya utajiri wake kwa ajili ya wenye mahitaji (philanthropic causes).

Kama ilivyo kwa wafanyabiashara wengine, ushindani ni suala la muhimu; Mo ameendelea kutoa ushindani kwa makampuni kama Coca Cola kwa kuzalisha kinywaji kipya cha Mo Cola.

Mpaka sasa Mo Dewji ndiye mtanzania pekee aliyepo kwenye orodha ya mabilionea wa dunia

Kwa mujibu wa Forbes, Elon Musk, Mark Zuckeberg na Jeff Bezos wanashika nafasi za juu za mabilionea duniani.

Wakati huo huo Forbes imemtaja Rais wa Shiriksho la Soka Barani Afrika Patrick Motsepe (63) kuwa ni Bilionea wa 1173.

Utajiri wa Motsepe wa Dola za Kimarekani 3 bilioni unafanya katika taifa lake la Afrika Kusini kushika nafasi ya nne akizidiwa na Koos Becker ambaye duniani anashika nafasi ya 1049, Nick Oppenheimmer & family nafasi ya 254 na tajiri namba moja nchini Afrika Kusini Johann Rupert & family anayeshika nafasi ya 164.

Aidha ni matajiri sita pekee kutoka Afrika Kusini ambao wapo katika orodha ya mabilionea wa dunia wa Forbes.

Credit to: Jabir Johnson/JAIZMELA/Forbes.

Thursday, March 6, 2025

Wanawake Moshi DC wazuru Gereza la Karanga; Wabubujikwa na machozi…

 

Baadhi ya wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wakikabidhi mahitaji kwa ajili ya Wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Karanga, Moshi katika ziara mnamo tarehe 6 Machi 2025. Msaada huo wa Hali na Mali ulipokelewa na SSP Rehema J. Okello kwa niaba ya Mkuu wa Gereza hilo. (Credit to: Jabir Johnson/ JAIZMELA)

Wanawake katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi wameonyesha umuhimu wa wa uungwaji mkono, usawa, na haki, baada ya kufanya ziara fupi katika Gereza la Karanga-Moshi huku wakidhihirisha huruma na utambuzi wa haki za binadamu.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kuhama kutoka KDC na kuingia makao mapya Sango wilayani humo pia kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 8 Machi ambapo Kitaifa yatafanyika jijini Arusha.

Akizungumza baada ya kuzuru Gereza la Karanga-Moshi Afisa Maendeleo na Mratibu wa Mikopo katika Halmashauri ya Moshi Bi. Stella Magori amesema kuenda kuwaona wafungwa na kuwasaidia kunaweza kuhamasisha jamii kuwa na mtazamo wa usawa na haki, na kwamba sio kila mtu alikosea kwa kiwango cha kuwa na adhabu ya kudumu na kwamba wafungwa wanastahili haki za kimsingi.

“Huu ni mwendelezo wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani, tumeona ni vema kusherehekea na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza la Karanga; wanawake wametoa michango mbalimbali ambayo imetumika kununua baadhi ya mahitaji kwa ajili ya wafungwa na mahabusu hao. Tuna la kujifunza ikiwamo kupata faraja kujimuika na kina mama wenzetu ambao hawapati nafasi ya kuwepo uraiani; kuna haja ya kwenda kuwafariji kila wakati,” amesema Bi. Stella Magori.

Akipokea msaada huo kutoka kwa wanawake wa Halmashauri ya Moshi kwa niaba ya Mkuu wa Gereza; SSP Rehema Okello wa Gereza la Karanga –Moshi amesema kitendo kilichofanywa na watumishi hao ni mfano wa kuigwa na kwamba wasisite kufanya hivyo na kuihamasisha jamii kujitolea kuwaona wafungwa na kuwatia moyo.

“Jambo mlilofanya ndugu zangu ni la kuigwa, nasi tunalipokea kwa mikono miwili kwani mnapokuja kuwaona wafungwa hawa mnawatia moyo n ahata wengine wakimaliza vifungo vyao watarudi kwenye jamii na kuwa watu wema, asanteni sana,” amesema SSP R.J Okello.

Wakizungumza kwa hisia kali wanawake walijionea hali halisi ya wafungwa katika gereza la Karanga –Moshi wamesema wamejifunza kuwa kutoa ni moyo na sio utajiri na kwamba kila mtu anastahili nafasi ya kurekebisha maisha yake, hata wale waliokosa bahati au walikosea.

Wakati mwingine, kusaidia wafungwa kunaweza kuleta mabadiliko chanya, kama vile kuongeza uelewa kuhusu haki za wafungwa, kuboresha masharti yao, na kutoa fursa za upya kwao baada ya kifungo. Hii inachangia katika kupunguza uhalifu na kusaidia mfungwa kuungana tena na jamii baada ya kutoka gerezani.







Jamii yatakiwa kutofumbia macho Ukatili wa Kijinsia; Moshi DC yashughulikia kesi 16 ndani ya miezi sita

Baadhi ya wanawake katika Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wakionyesha nyuso za furaha kudhihirisha uwepo wao na matamkombalimbali kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8. Mnamo Machi 5, 2025 wanawake wa Halmshauri ya Wilaya ya Moshi walikusanyika katika Viwanja vya KDC kuadhimisha siku hiyo kabla ya kuelekea Jijini Arusha ambako sherehe hizo zitafanyika kitaifa. (Credit to: Jabir Johnson/ JAIZMELA)

 Jamii imetakiwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyotendea wanawake na wasichana katika Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro ili kutokomeza changamoto hiyo na kujenga taifa bora linalosimamia haki na usawa.

Rai hiyo imetolewa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Ulimwenguni ambayo hufanyika kila Machi 8 ambayo nchini Tanzania mwaka huu wa 2025 inafanyika Jijini Arusha.

Akizungumza na hadhira ya wanawake katika Halmashauri ya Moshi mnamo Machi 5 katika viwanja vya KDC wilayani humo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Komredi Godfrey Mnzava amesema mpaka sasa hatua katika kushughulikia ukatili wa kijinsia imepigwa kuelekea kuitokomeza kabisa.

DC Mnzava amesema kumekuwa na tabia ambayo nivema idhibitiwe ya kumalizana wenyewe kwa wenyewe katika jamii pindi mwanamke au msichana anapofanyiwa vitendo vya ukatili hatua ambayo imekuwa ikivuta shati juhudi za serikali na wadau mbalimbali katika kumpigania mwanamke na msichana.

Akiwasilisha ripoti kuhusu Wanawake katika Halmshauri ya Moshi Afisa Maendeleo Stella Magori amesema jamii inapaswa kuendelea kutoa ulinzi kwa watoto wa kike kwani ndani ya kipindi kifupi matukio hayo yametokea.

“Ingawa juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia zinaendelea, lakini bado watoto wa kike wanatendewa vitendo vya ukatili ambapo Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Februari 2025  watoto wa kike 16 walifanyiwa ukatili wa kijinsia na matukio hayo yaliripotiwa katika vyombo vya kisheria ambapo matukio 13 yameshatolewa hukumu na mengine matatu yanaendelea mahakama,” amesema Bi. Magori

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Morris Makoi ametaka ushirikiano baina yake na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kuhusu elimu ya biashara ili kuwasaidia wanawake wanapoenda kukopa mikopo wawe wana ufahamu kuhusu fedha watakazopata watazifanyia kitu gani kwa ustawi wao na jamii kwa ujumla.

Awali DC Mnzava alishuhudia Bonanza la Michezo ikiwa sehemu ya  kionjo katika kuadhimisha siku ya mwanamke, michezo kama kukimbiza kuku, kukimbia na magunia na kukimbia na yao katika kijiko kikiwa mdomoni ilikuwa ni burudani tosha kutoka kwa wanawake.

Pia mashindano ya unywaji wa soda katika bonanza hilo ambalo DC Mnzava aliwakabidhi washindi wa michezo hiyo vyeti vya kutambua mchango wao na Shilingi 10,000/= kila mmoja ambapo jumla ya washindi wapatao 15 walijipatia zawadi hizo kwenye bonanza hilo.

Kwa upande wao washiriki wa Siku hiyo iliyopambwa kwa Kauli mbiu, “Wanawake na Wasichana 2025, Haki, Usawa na Uwezeshaji,” wamesema ushiriki wa mwanamke katika kuijenga jamii ni mkubwa hivyo mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ni vema yakaendelea ili kujenga jamii iliyo bora.