Watu watatu
wamefariki dunia kutokana na ajali iliyohusisha gari dogo na mabasi mawili ya
Abiria mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kwa kile kinasadikika ni mwendokasi na
kuovertake.
Jeshi la
Polisi mkoani Kilimanjaro lilifika eneo la Kaanan, mjini hapa ilipotokea ajali
hiyo kwa ajili ya uokoaji ambapo gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba za
usajili T 592 EKU iligongana uso kwa uso na basi la Esta Luxury Coach tana na
changamoto hiyo katika barabara ya Moshi- Arusha ikitokea Himo.
Mashuhuda wa
tukio hilo wanasema mabasi ya abiria ya Kidia na Esta Luxury Coach ndio chanzo
cha ajali hiyo baada ya Kidia kushindwa kumaliza kulipita gari la Esta ambapo Rav
4 ilikutana uso kwa uso na basi la Esta.
Mkuu wa
Wilaya ya Moshi Godfrey Mzava amesema ajali hiyo ilitokea leo saa 12:30 asubuhi
na kwamba abiria waliokuwepo katika basi la Esta walipatiwa basi jingine
kuendelea na safari ya Dar es Salaam.
Miili ya
Marehemu iliyokuwemo katika Rav 4 imehifadhiwa katika Hospitali ya Kanda ya
Rufaa ya KCMC kwa ajili ya uchunguzi zaidi na taratibu nyingine za mazishi.
0 Comments:
Post a Comment