Tuesday, February 4, 2025

Bweni la wanafunzi Kaloleni Islamic Seminary laungua moto

Chumba cha tatu cha Bweni la Makka katika shule ya Kaloleni Islamic Smeinary baada ya kuzimwa kwa moto. Picha na Jabir Johnson/JAIZMELA correspondent

Zaidi ya wanafunzi 50 wa kike, Shule ya Sekondari ya Kaloleni Islamic ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kuungua na moto baada ya bwenì walilokuwa wakiishi kulipuka moto leo saa saba mchana.

Taarifa za wafanyakazi na majirani wa karibu na shule hiyo ndio waliofanikisha ujio wa haraka wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambalo lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto katika bweni hilo la wasichana lenye vyumba 20.

Wakiwa katika huzuni kuu kutokana na viaa vyao kuungua moto, Wanafunzi wa kike shuleni hapo walipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo ambapo lamic

Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni wanafunzi wa chumba cha tatu ndani ya bweni kilicholipuka moto kuwa na vifaa vinavyolipuka.

Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jeremiah Mkomagi amesema hakuna majeruhi yaliyojitokeza licha ya vifaa vya wanafunzi yakiwamo madaftari, magodoro.

“Majira ya saa 7 na dakika 17 mchana tulipata taarifa za tukio la moto katika shule hii kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Urio, kikosi kilichokuwepo zamu kilifika na kusaidiana na wafanyakazi na majirani kuzima moto,” alisema Mkomagi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Mohammed Hussein Migeto amesema wakati tukio la moto linajitokeza alikuwa nje ya shule na alirudi haraka na kuchukua hatua stahiki kuhakikisha wanafunzi wapo salama licha ya wawili miongoni mwao kupata mshtuko na kukimbizwa hospitalini.

“Wanafunzi wawili walipata mshtuko baada ya kusikia kelele za moto kutokana kwa wanafunzi wenzao wakati wakiwa msikitini,…” aliongeza Mwalimu Migeto.

Hii ni mara ya pili kwa shule hiyo ya Kiislamu kupatwa na janga la moto; Moto katika shule unaweza kuwa na athari kubwa kwa jamii nzima; Jamii inaweza kukosa huduma muhimu za elimu kwa wanafunzi ambao wanashindwa kurudi shule kwa sababu ya uharibifu unaojitokeza wakati wa majanga ya moto.









0 Comments:

Post a Comment