Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Tuesday, February 4, 2025

Bweni la wanafunzi Kaloleni Islamic Seminary laungua moto

Chumba cha tatu cha Bweni la Makka katika shule ya Kaloleni Islamic Smeinary baada ya kuzimwa kwa moto. Picha na Jabir Johnson/JAIZMELA correspondent

Zaidi ya wanafunzi 50 wa kike, Shule ya Sekondari ya Kaloleni Islamic ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kuungua na moto baada ya bwenì walilokuwa wakiishi kulipuka moto leo saa saba mchana.

Taarifa za wafanyakazi na majirani wa karibu na shule hiyo ndio waliofanikisha ujio wa haraka wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambalo lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto katika bweni hilo la wasichana lenye vyumba 20.

Wakiwa katika huzuni kuu kutokana na viaa vyao kuungua moto, Wanafunzi wa kike shuleni hapo walipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo ambapo lamic

Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni wanafunzi wa chumba cha tatu ndani ya bweni kilicholipuka moto kuwa na vifaa vinavyolipuka.

Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la tukio Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jeremiah Mkomagi amesema hakuna majeruhi yaliyojitokeza licha ya vifaa vya wanafunzi yakiwamo madaftari, magodoro.

“Majira ya saa 7 na dakika 17 mchana tulipata taarifa za tukio la moto katika shule hii kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Urio, kikosi kilichokuwepo zamu kilifika na kusaidiana na wafanyakazi na majirani kuzima moto,” alisema Mkomagi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Mohammed Hussein Migeto amesema wakati tukio la moto linajitokeza alikuwa nje ya shule na alirudi haraka na kuchukua hatua stahiki kuhakikisha wanafunzi wapo salama licha ya wawili miongoni mwao kupata mshtuko na kukimbizwa hospitalini.

“Wanafunzi wawili walipata mshtuko baada ya kusikia kelele za moto kutokana kwa wanafunzi wenzao wakati wakiwa msikitini,…” aliongeza Mwalimu Migeto.

Hii ni mara ya pili kwa shule hiyo ya Kiislamu kupatwa na janga la moto; Moto katika shule unaweza kuwa na athari kubwa kwa jamii nzima; Jamii inaweza kukosa huduma muhimu za elimu kwa wanafunzi ambao wanashindwa kurudi shule kwa sababu ya uharibifu unaojitokeza wakati wa majanga ya moto.









Saturday, February 1, 2025

Watatu wafariki dunia papo hapo kwa ajali mjini Moshi

 

Watu watatu wamefariki dunia kutokana na ajali iliyohusisha gari dogo na mabasi mawili ya Abiria mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kwa kile kinasadikika ni mwendokasi na kuovertake.

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro lilifika eneo la Kaanan, mjini hapa ilipotokea ajali hiyo kwa ajili ya uokoaji ambapo gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba za usajili T 592 EKU iligongana uso kwa uso na basi la Esta Luxury Coach tana na changamoto hiyo katika barabara ya Moshi- Arusha ikitokea Himo.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mabasi ya abiria ya Kidia na Esta Luxury Coach ndio chanzo cha ajali hiyo baada ya Kidia kushindwa kumaliza kulipita gari la Esta ambapo Rav 4 ilikutana uso kwa uso na basi la Esta.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godfrey Mzava amesema ajali hiyo ilitokea leo saa 12:30 asubuhi na kwamba abiria waliokuwepo katika basi la Esta walipatiwa basi jingine kuendelea na safari ya Dar es Salaam.

Miili ya Marehemu iliyokuwemo katika Rav 4 imehifadhiwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya uchunguzi zaidi na taratibu nyingine za mazishi.