Tundu Antipas Lissu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Tundu Lissu ni mwanasheria maarufu nchini Tanzania, na aliwahi kuwa Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika(TLS), mwaka 2020 aligombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema na kushindwa na mgombea wa chama tawala John Magufuli, aliyefariki dunia Machi 2021.
Lissu aliyenusurika kifo Septemba 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi mjini Dodoma, ni maarufu kwa siasa za mapambano na ''ulimi mkali'' hali ambayo mara imemuweka katika mabishano makali na wanasiasa wezake hususan wa chama tawala. Amekuwa akisema alipopigwa risasi alikuwa ''nusu mfu''
Kuanzia mwaka 2010 Lissu alikuwa mbunge wa Singida Mashariki
na alijipatia umaarufu kwa michango yake bungeni hususan ya kuikosoa serikali
ya Rais Jakaya Kikwete na baadaye Hayati Rais John Pombe Magufuli.
Lissu ni msomi wa kiwango cha shahada ya umahiri aliyoipata nchini Uingereza katika Chuo Kikuu cha Warwick kati ya mwaka 1995 na1996. Kabla ya hapo alipata shahada ya kwanza ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikohitimu mwaka 1994.
Maisha yake yamekuwa zaidi katika harakati za kutetea haki za
binadamu na kutoa msaada wa kisheria kwa watu wenye mahitaji lakini wana uwezo
mdogo wa kifedha. Aliwahi pia kuwa mwenyekiti wa chama wanasheria za Mazingira
Tanzania (LIT) katika miaka ya 1990.
0 Comments:
Post a Comment