Mstahiki Meya Mstaafu wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu ametoa msaada wa Hali na Mali katika Kituo cha Watoto waishio katika mazingira duni na Yatima cha Upendo Foundation and Child Light.
JR ambaye ni diwani wa Bomambuzi ametoa msaada huo
ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika iliyopata kutoka
kwa Uingereza.
Juma Rahibu amesema kuwasaidia watoto ni suala la
Upendo ambalo kila mtanzania anapaswa kuwa nalo ili kujenga Taifa Bora
Aidha Juma Rahibu amewataka watoto hao na wadau wa
kusaidia watoto kuendelea kumwamini Mungu kwani ndiye Mkuu na mwenye uwezo wa
kufanikisha mambo yao
“Hakuna cheo kikubwa dunia zaidi ya upendo, hawa
watoto mnawendeleza leo mnawasimamia, baadhi hawana wazazi wengine mmewatoa
katika mazingira duni mzazi wao yupo ni Mungu Mkuu na mpigie makofi Mungu huyu,”
alisema Juma Rahibu.
Katika hafla hiyo ya shukrani kwa Mungu na kwa
wadau mbalimbali kituoni hapo Soweto mjini Moshi ilianza kwa NENO la Mungu
kutoka kwa Mchungaji Elia Ngayange wa Kanisa la Moravian
“Ni jambo la thamani mbele za Mungu hasa
unapohusika kuyawezesha makundi maalum kufikia malenngo yao, Mungu huwa
analithamini sana jambo hilo,” alisema Mchungaji Nyagyange.
Katika risala ya watoto kwa Mgeni rasmi wamesema
mafanikio wameyapata kutoka kwa watu mbalimbali ikiwamo Elimu bora licha ya
kwamba msaada mkubwa unahitajika kwa ajili ya kuwainua zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upendo Foundation and Child
Light Faith Nelson amesema Kituo chale kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya
watoto kukosa bima za Afya hivyo mtoto anapougua inabidi kutafuta pesa kwa
ajili ya matibabu.
Kituo hicho cha Watoto waishio maisha duni kina watoto 24
ambao wamekuwa wakilelewa na kupatiwa huduma za malazi, mavazi, chakula na
elimu bora.
Kwa upande wake Vanessa Michael amesema Upendo
Foundation and Child Light inawasaidia kufikia malengo.
Kiasi cha shilingi milioni moja ikiwamo ahadi kimepatikana katika hafla hiyo ya shukrani, huku Meya huyo Mstaafu amechangia kiasi cha shilingi 520,000/- kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Kituo hicho kulea watoto hao.
0 Comments:
Post a Comment