Christine A. Kimaro baada ya kupokea Komunyo ya kwanza katika Parokia Teule Jina Takatifu la Maria, Mnazi Mmoja-Moshi mkoani Kilimanjaro. |
Ekaristi Takatifu ni ishara ya Umoja na kifungo cha mapendo, karamu ya pasaka ambamo waamini humpokea Kristo na roho hukazwa neema na kupewa Amana ya uzima wa milele.
Shangwe, nderemo, bashasha na vigelegele vilitawala baada ya Christine Kimaro
kupata komunyo yake ya kwanza katika Parokia Teule Jina Takatifu la
Maria, Mnazi Mmoja-Moshi mkoani Kilimanjaro.
Christine mwenye umri wa miaka 11 ni miongoni mwa watoto takribani 50 waliopata
komunyo ya kwanza mnamo Desemba 26,2023 katika Kanisa hilo.
Katika hafla hiyo Baba Paroko Ludà si Retembea aliwapongeza watoto hao na
kuwataka kuishi kama Kristo Yesu alivyoagiza na mafundisho waliyoyapata.
Kwa upande wake Padre Mark aliwapongeza watoto hao kwa kupokea komunyo hiyo, na
kuwataka kujifunza kumtegemea Mungu.
Aidha hafla hiyo iliendelea kwa mtoto Christine kufanyiwa sherehe ya kumpongeza
kutokana na hatua aliyofikia
Ndugu, jamaa na marafiki walimiminika katika ukumbi wa Police Line mjini Moshi
ambako walisheherekea pamoja.
Babu, Bibi, mashangazi na wajomba walikuwepo katika hafla hiyo ambapo
walimtunuku zawadi mbalimbali mtoto Christine.
Hakika ilifana, mtoto Christine alianza kwa kuwakaribisha ndugu, jamaa na
marafiki kisha Wazazi walipata fursa ya kuzungumza na wageni waalikwa.
Pia keki ilikatwa, mtoto Christine aliikata na kuwalisha wageni wote
waalikwa waliokuwepo ukumbi hapo.
Babu wa Christine alitoa shukrani zake za dhati kwa wageni wote
Hata hivyo Majirani wa Familia ya Christine hawakuwa nyuma walimtunuku
Christine na Wazazi wake zawadi ambazo hakika zilionyesha ujirani mwema.
Haikutosha muda wa maakuli na matojoro uliwadia Christine aliongoza msururu wa
watu kupata kilichoandaliwa kwa ajili yao
Hatimaye baba mzazi wa Christine, Mzee Kimaro alitoa neno la shukrani kwa
wageni waalikwa.
Hakika Desemba 26,2023 haitasahaulika katika Kumbukumbu ya wote waliohudhuria
hafla ya kumpongeza mtoto Christine kwa kupata Komunyo yake ya kwanza.
0 Comments:
Post a Comment