Sunday, August 13, 2023
Friendly Veterans Match: HIMO 1-4 BEST MARIDADI
Mchezo wa kiveterani baina ya Himo dhidi ya Best Maridadi zote za Moshi mkoani Kilimanjaro umemalizika kwa wenyeji Himo kuzabuliwa kwa mabao 4-1 na Best Maridadi.
Hadi kipindi
cha kwanza kinamalizika ilikuwa ni sare ya 1-1, hata hivyo kipindi cha pili
kilikuwa shubiri kwa wenyeji kuruhusu wavu wake kutikiswa mara tatu nyingine.
Uongozi wa
Himo umesema sababu za kupoteza mchezo huo ni uwepo wa vijana wengi katika timu
ya Best Maridadi jambo ambalo hawajafurahishwa nao kwani vijana hao walitakiwa
kuwa kwenye mechi za ushindani kukuza vipaji vyao.
Kwa upande
wa Best Maridadi wamekiri kuwatumia vijana wengi kipindi cha pili kutokana na
kukosekana kwa wachezaji wake.
Hata hivyo
wamesema watalifanyia kazi walau wawe na vijana wanne kwa ajili ya kuungana na
maveterani hao ili kuchezo soka.
Tuesday, August 8, 2023
Posta Kilimanjaro yajadili mipango iliyotekeleza 2022-2023
Wafanyakazi wa Posta mkoa wa Kilimanjaro katika picha ya pamoja baada ya kujadili waliyoyafanya kwa mwaka 2022-2023 |
Wafanyakazi
wa Shirika la Posta Tanzania mkoa wa Kilimanjaro wamefanya kikao kwa ajili ya
kujadili namna walivyotekeleza bajeti ya mwaka wa fedha uliopita 2022-2023 na
kujipanga katika bajeti ya mwaka 2023-2024.
Meneja
wa shirika la Posta mkoa wa Kilimanjaro Deodatus Ako, ameyasema hayo
Agost 8 mjini Moshi wakati akisoma taarifa yake ya utendaji kazi ya mwaka
2022-2023 ambayo ilikuwa ikiangazia mafanikio na changamoto zake.
Katika
hotuba hiyo Ako, amewasihi watumishi kufanyakazi kwa kuzingatia weledi na kuona
namna gani wanaweza kutatua changamoto zilizopo ili sekta hiyo iweze kuchangia
zaidi kwenye pato la taifa.
Meneja
huyo amesema kikao hicho ni muhimu kwa kuwa watumishi wanashirikishwa kwa
uwazi kuhusu namna walivyotekeleza bajeti ya mwaka 2022-2023 na kujipanga
katika bajeti ya mwaka 2023-2024.
Aidha
amesema katika kikao hicho pia wamesainiana mikataba ya utendaji kati ya meneja
wa mkoa na wafanyakazi wa shirika la Posta ili waweze kuwajibika katika maeneo
yao ya kazi.
Kwa
upande wake Meneja Masoko wa Shirika la Posta mkoa wa Kilimanjaro Mwanamkuu
Mussa, amesema anuani za makazi zimesaidia kurahisisha utambuzi wa utoaji wa
huduma za posta nchini
Amebainisha
kuwa mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania imesaidia utoaji wa huduma sio tu
kwa shirika la Posta na ufikishaji wa vifurushi na vipeto katika maeneo
ya makazi, ofisi na sehemu za biashara.
Naye Posta Master Wilaya ya Mwanga Ally Kilemile, amesema mikataba ya kazi ambayo wameisaini itawasaidia kuongeza ari ya utendaji kazi mahapa ka kazi ili malengo waliyojiwekea katika kipindi cha mwaka 2023-2024 yaweze kufanikiwa ufanisi mkubwa.
Katika semina hiyo pia zilitolewa mada mbalimbali ikiwemo mada ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza zilizotolewa na Wauguzi kutoka KCMC kitengo cha Afya ya Jamii na ambapo pia walipatiwa mafunzo ya Biashara na Masoko kutoka kwa mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.