Thursday, December 28, 2023
Christine Kimaro apata Komunyo ya Kwanza
Christine A. Kimaro baada ya kupokea Komunyo ya kwanza katika Parokia Teule Jina Takatifu la Maria, Mnazi Mmoja-Moshi mkoani Kilimanjaro. |
Ekaristi Takatifu ni ishara ya Umoja na kifungo cha mapendo, karamu ya pasaka ambamo waamini humpokea Kristo na roho hukazwa neema na kupewa Amana ya uzima wa milele.
Shangwe, nderemo, bashasha na vigelegele vilitawala baada ya Christine Kimaro
kupata komunyo yake ya kwanza katika Parokia Teule Jina Takatifu la
Maria, Mnazi Mmoja-Moshi mkoani Kilimanjaro.
Christine mwenye umri wa miaka 11 ni miongoni mwa watoto takribani 50 waliopata
komunyo ya kwanza mnamo Desemba 26,2023 katika Kanisa hilo.
Katika hafla hiyo Baba Paroko Ludà si Retembea aliwapongeza watoto hao na
kuwataka kuishi kama Kristo Yesu alivyoagiza na mafundisho waliyoyapata.
Kwa upande wake Padre Mark aliwapongeza watoto hao kwa kupokea komunyo hiyo, na
kuwataka kujifunza kumtegemea Mungu.
Aidha hafla hiyo iliendelea kwa mtoto Christine kufanyiwa sherehe ya kumpongeza
kutokana na hatua aliyofikia
Ndugu, jamaa na marafiki walimiminika katika ukumbi wa Police Line mjini Moshi
ambako walisheherekea pamoja.
Babu, Bibi, mashangazi na wajomba walikuwepo katika hafla hiyo ambapo
walimtunuku zawadi mbalimbali mtoto Christine.
Hakika ilifana, mtoto Christine alianza kwa kuwakaribisha ndugu, jamaa na
marafiki kisha Wazazi walipata fursa ya kuzungumza na wageni waalikwa.
Pia keki ilikatwa, mtoto Christine aliikata na kuwalisha wageni wote
waalikwa waliokuwepo ukumbi hapo.
Babu wa Christine alitoa shukrani zake za dhati kwa wageni wote
Hata hivyo Majirani wa Familia ya Christine hawakuwa nyuma walimtunuku
Christine na Wazazi wake zawadi ambazo hakika zilionyesha ujirani mwema.
Haikutosha muda wa maakuli na matojoro uliwadia Christine aliongoza msururu wa
watu kupata kilichoandaliwa kwa ajili yao
Hatimaye baba mzazi wa Christine, Mzee Kimaro alitoa neno la shukrani kwa
wageni waalikwa.
Hakika Desemba 26,2023 haitasahaulika katika Kumbukumbu ya wote waliohudhuria
hafla ya kumpongeza mtoto Christine kwa kupata Komunyo yake ya kwanza.
Monday, December 18, 2023
Uhamiaji Tanzania, Uhamiaji China zatiliana saini kuimarisha uhusiano wa kibiashara na ulinzi
Jeshi la Uhamiaji Tanzania na Jeshi la Uhamiaji la Jamhuri ya Watu wa China zimetilia saini hati za makubaliano ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara, ulinzi na Uhamiaji baina ya mataifa hayo mawili.
Wednesday, December 13, 2023
Zahara is no more. Dies at age of 36
Tuesday, December 12, 2023
Askofu Malasusa, Mhashamu Ludovick Minde wakutana
Mkuu wa Kanisa Mteule wa KKKT Askofu Alex Malasusa na Mhashamu Askofu Ludovick Minde wa Kanisa Katoliki wakiteta jambo katika siku ya maziko ya Askofu Mstaafu Erasto Kweka. |
Viongozi wa dini wana ustawi wa jamii zao katika moyo. Viongozi wa dini wanahitaji kufahamu mambo mapya kuhusu masuala yanayowakabili waumini wao. Ni wajibu wako kuhakikisha kwamba haki zote za watoto na vijana zinaungwa mkono ili waweze kufanya maamuzi kwa kuwa na taarifa na kwa kuwajibika na kuishi kwa afya, uzazi na maisha yenye ukamilifu.
Saturday, December 9, 2023
MIAKA 62 YA UHURU WA TANGANYIKA: Juma Raibu atoa msaada Kituo cha Watoto Yatima Soweto-Moshi
Mstahiki Meya Mstaafu wa Manispaa ya Moshi Juma Raibu ametoa msaada wa Hali na Mali katika Kituo cha Watoto waishio katika mazingira duni na Yatima cha Upendo Foundation and Child Light.
JR ambaye ni diwani wa Bomambuzi ametoa msaada huo
ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika iliyopata kutoka
kwa Uingereza.
Juma Rahibu amesema kuwasaidia watoto ni suala la
Upendo ambalo kila mtanzania anapaswa kuwa nalo ili kujenga Taifa Bora
Aidha Juma Rahibu amewataka watoto hao na wadau wa
kusaidia watoto kuendelea kumwamini Mungu kwani ndiye Mkuu na mwenye uwezo wa
kufanikisha mambo yao
“Hakuna cheo kikubwa dunia zaidi ya upendo, hawa
watoto mnawendeleza leo mnawasimamia, baadhi hawana wazazi wengine mmewatoa
katika mazingira duni mzazi wao yupo ni Mungu Mkuu na mpigie makofi Mungu huyu,”
alisema Juma Rahibu.
Katika hafla hiyo ya shukrani kwa Mungu na kwa
wadau mbalimbali kituoni hapo Soweto mjini Moshi ilianza kwa NENO la Mungu
kutoka kwa Mchungaji Elia Ngayange wa Kanisa la Moravian
“Ni jambo la thamani mbele za Mungu hasa
unapohusika kuyawezesha makundi maalum kufikia malenngo yao, Mungu huwa
analithamini sana jambo hilo,” alisema Mchungaji Nyagyange.
Katika risala ya watoto kwa Mgeni rasmi wamesema
mafanikio wameyapata kutoka kwa watu mbalimbali ikiwamo Elimu bora licha ya
kwamba msaada mkubwa unahitajika kwa ajili ya kuwainua zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upendo Foundation and Child
Light Faith Nelson amesema Kituo chale kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya
watoto kukosa bima za Afya hivyo mtoto anapougua inabidi kutafuta pesa kwa
ajili ya matibabu.
Kituo hicho cha Watoto waishio maisha duni kina watoto 24
ambao wamekuwa wakilelewa na kupatiwa huduma za malazi, mavazi, chakula na
elimu bora.
Kwa upande wake Vanessa Michael amesema Upendo
Foundation and Child Light inawasaidia kufikia malengo.
Kiasi cha shilingi milioni moja ikiwamo ahadi kimepatikana katika hafla hiyo ya shukrani, huku Meya huyo Mstaafu amechangia kiasi cha shilingi 520,000/- kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Kituo hicho kulea watoto hao.