Mtoto anayefahamika kwa jina la Laurent Simons (8) anatarajiwa kujiunga na masomo ya Chuo Kikuu nchini Ubelgiji baada ya kumaliza masomo ya sekondari kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.
Simons ambaye wazazi wake ni kutoka nchini Uholanzi alipata diploma yake kwenye darasa la wanafunzi wenye miaka 18.
Kinachoelezwa na wazazi wake ni kwamba mtoto huyo wa kiume ana uwezo wa juu wa akili (IQ) na kwamba somo analolipenda sana ni hesabu kwasababu ni pana.
Kwa sasa yupo likizo ya miezi miwili kabla ya kujiunga na masomo ya shahada nchini humo.
Baba wa mtoto huyo alikaririwa na kituo cha redio cha RTBF nchini Ubelgiji akisema mtoto huyo alipata wakati mgumu akiwa mdogo wakati wa kucheza na wenzake na hakufurahishwa na vifaa vya kuchezea.
"Ikiwa ataamua kesho kuwa seremala, hilo halitakuwa tatizo kwetu kama atakuwa na furaha," alisema baba yake.
Laurent Simons |

Laurent Simons akiwa na wazazi wake. |
0 Comments:
Post a Comment