Monday, July 2, 2018

Andres Manuel Lopez Obrador: Rais mpya wa Mexico, Trump ampongeza

Mgombea wa siasa za mrengo wa kushoto nchini Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador amepata ushindi mkubwa baada ya kuchaguliwa kuwa rais kwa asilimia 53 ya kura, tume ya uchaguzi imearifu.
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador


Matokeo hayo ya awali yamezingatia idadi ya kura zilizokusanywa kutoka kwa wawakilishi kwenye vituo 7,800 vya kupigia kura. 


Rais wa taasisi ya kitaifa ya uchaguzi Lorenzo Cordova amethibitisha matokeo hayo.
Amesema, Lopez Obrador ameshinda kwa kati ya asilimia 53 na 53.8 ya kura zote, wakati mgombea wa chama cha kihafidhina wa sera za wastani, Ricardo Anaya akipata wingi wa kura wa hadi asilimia 22.8, na Jose Antonio Meade anayetokea chama cha rais anayeondoka madarakani Enrique Pena Nieto cha Institutional Revolutionary, PRI akiambulia hadi asilimia 16.3 tu ya kura zote.

Obrador akisalimiana na wafuasi wake wakati wa Kampeni za Uchaguzi uliomweka madarakani na kumuondoa Enrique Peña Nieto.
Rais wa Marekani, Donald Trump amempongeza Obrador kwa ushindi huo aliouita wa kishindo akisema, ana matarajio makubwa ya kushirikiana na kiongozi huyo.

0 Comments:

Post a Comment