Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Faraja Nguka amewataja washtakiwa hao kuwa ni dereva mkazi wa Mbezi Luis, Kefas Mlenzi (30), Polisi Jamii, Juma Mtali (35) na Polisi Jamii, Greyson Muhapa maarufu kama Masu (32) wote wakati wa Mbezi Luis.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Ally Salum, wakili Nguka amedai Juni 28 mwaka huu huko Mbezi katika Wilaya ya Ubungo washtakiwa kwa pamoja walikamatwa wakiwa na vipande 30 vya meno ya tembo vyenye thamani USD 105,000 sawa na Sh 239,505,000 bila ya kuwa na Kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori.
Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi za uhujumu uchumi, isipokuwa mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 23, 2018 kwa mijibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.