Yousafzai Malala |
Anafahamika kwa
harakati zake za uwakili wa haki za binadamu hususani katika masuala ya elimu
kwa wanawake kwa wenyeji wa bonde la Swat huko Khyber Pakhtunkhwa Kaskazini
Magharibi mwa Pakistan .
Malala na tuzo yake |
Kundi linalodaiwa la kigaidi na ulimwengu wa magharibi la Taliban liliwazuia
wasichana katika eneo hilo
wasihudhurie masomo. Uwakili wake wa kuwatetea wasichana wa eneo hilo ulikua hadi kufikia
medani ya Kimataifa.
Yousafzai alizaliwa katika mji wa kibiashara wa Mingora
huko Pakistan .
Familia yake ilikuwa na shule katika eneo hilo .
Binti huyo alidai kuwa Jinnah na Benazir Bhutto ni role-models wake katika harakati
zake. Aidha Yousafzai alisema mawazo ya baba yake na kazi zake za kiutu
zilimmwongezea hamasa.
Mapema mwaka 2009 akiwa na kati ya miaka 11-12 aliandika
katika blogu ya BBC kwa lugha ya Urdu akielezea maisha yake na ukandamizwaji
unaofanywa na Taliban katika bonde hilo
la Swat. Msimu uliofuata mwandishi wa habari Adam B. Ellick wa New York Times
alitengeneza makala kuhusu maisha yake baada ya Jeshi la Pakistan kuingia katika eneo hilo .
Alionekana katika runinga na majarida mbalimbali na baadaye akapata
fursa ya kuwa mshiriki wa Tuzo ya Kimataifa ya Amani kwa Watoto iliyotolewa na
Mwanaharakati Desmond Tutu. Mchana wa Okotoba 9, 2012 Yousafzai alijeruhiwa
katika jaribio la kutaka kumuua lililolengwa na Taliban. Binti huyo alipoteza
fahamu na kupelekwa hospitalini kwenye Taasisi ya Cardiology ya Rawalpindi lakini baadaye alipata ahueni kisha kupelekwa
katika Hospitali ya Queen Elizabeth iliyopo Birmingham nchini
Uingereza.
Kitendo hicho cha Talibani cha kutaka kumuua binti huyo kiliibua
vuguvugu la kimataifa la kumuunga mkono Yousafzai. Januari 2013 Deutsche Welle
iliandika katika makala na taarifa zake kuwa
Yousafzai ni chipukizi anayefahamika zaidi ulimwenguni. Majuma machache
baada ya jaribio la kutaka kumuua Yousafzai
kundi la Waislamu 50 nchini Pakistan liliongoza ibada ya fatwā kwa waliotaka kufanya jaribio la mauaji kwa
binti huyo.
Tuzo mbalimbali alipokea ikiwamo ya Sakharov mwaka 2013 na mwaka
2014 alipokea Tuzo ya Amani ya Nobel.
Mwaka 2017 ametunukiwa uraia wa heshima wa Kanada.
0 Comments:
Post a Comment