Saturday, July 24, 2021

Msuya akambidhi Tadayo madaraka ya Kichifu

Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Cleopa David Msuya akimkabidhi fimbo ya Uchifu wa Mwanga Mbunge wa eneo hilo Joseph Tadayo katika hafla iliyofanyika Julai 24, 2021. (Picha na JAIZMELA/Kija Elias)
 

Waziri  Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Cleopa Msuya amekabidhi fimbo kama ishara ya kumwachia madaraka  Mbunge wa Mwanga Joseph Tadayo katika hafla iliyofanyika katika viwanja wa CCM wilayani humo Julai 24, 2021.

Akimkabidhi fimbo hiyo Msuya alimtaka Mbunge huyo kwenda  kushughulikia changamoto za wananchi wa wilaya hiyo ikiwamo kujengwa kwa hospitali ya Wilaya ya Mwanga pamoja na kuujenga mji huo uwe na hadhi kamili inayotakiwa.

“Nimekukabidhi fimbo hii ikakuongoze katika utawala wako, wananchi walikuamini wakakupa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo. Mimi wakati nikiwa mbunge na waziri walinipa jina la Baba wa Mwanga, na wewe fimbo hii inapotembea nayo ikakuongoze kama kiongozi, nenda kasikilize matatizo ya wananchi yatatue,” alisema Msuya.

Msuya alimtaka Mbunge Tadayo kushughulikia matatizo ya kimsingi ambayo yalishindikana kutatulika katika kipindi cha nyuma.

Awali akimsimika kijadi Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mwanga Maomboleo Mshana, alimkumbusha Mbunge huyo kuhusu kuwaunganisha watu wote ili kutunza Umoja wa Kitaifa.

Utamaduni huo wa kukabidhiana utawala wa kichifu hufanyika katika ardhi hiyo ikiwa ni ishara ya mwendelezo wa mamlaka kila baada ya kipindi fulani kwa mtu wa kabila la Wasangi na Wagweno. 


 


 

0 Comments:

Post a Comment