Monday, June 7, 2021

MAKTABA YA JAIZMELA: Abubakar Shekau ni nani?

Jina lake halisi ni Abu Mohammed Abubakar bin Mohammad al-Sheikawi; pia amekuwa akifahamika kwa jina la Darul Akeem wa Zamunda Tawheed. Jina lake halisi ni Abu Mohammed Abubakar bin Mohammad al-Sheikawi; pia amekuwa akifahamika kwa jina la Darul Akeem wa Zamunda Tawheed.

Juni 6, 2021 Kundi la Kijeshi la Kiislamu la Afrika Magharibi (ISWAP) limesema katika mkanda wa sauti ambao umekaririwa na vyombo vya habari vya kimataifa kuwa Kiongozi wa Kundi la Boko Haram la Nigeria, Abubakar Shekau amefariki dunia.

Taarifa zinasema Shekau alifariki dunia Mei 18 mwaka huu kwa kujilipua kwa bomu baada ya kuwa anafuatiliwa na wapiganaji wa ISWAP.

Sauti ambayo inadhaniwa kuwa ni ya mpinzani wake Abu Musab al-Barnawi ambaye ni kiongozi wa ISWAP ilisema, “ Abubakar Shekau, Mungu ameshamhukumu kwa kumpeleka peponi.”

Watu wawili wanaomfahamu al-Barnawi walithibitisha kuwa sauti iliyokuwa ikisikika katika mkanda huo ilikuwa ya kiongozi huyo wa ISWAP.

Idara ya usalama ya Nigeria katika taarifa yake iliyothibitishwa na watafiti wa Boko Haram ilisema Shekau amefariki dunia katika misitu ya Sambisa.

ABUBAKAR SHEKAU NI NANI?

Jina lake halisi ni Abu Mohammed Abubakar bin Mohammad al-Sheikawi; pia amekuwa akifahamika kwa jina la Darul Akeem wa Zamunda Tawheed.

Tarehe za kuzaliwa kwake zinatofautiana, kuna ripoti zinasema alizaliwa mnamo mwaka 1965, 1969 na nyingine zinasema alizaliwa mnamo mwaka 1973 au 1975. Shekau mzaliwa wa Yobe huko Nigeria amefariki dunia akiwa na umri kati ya miaka 46 na 56.

Alikuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram baada ya mtangulizi wake Ustaz Mohammed Yusuf kuhukumiwa kifo mnamo mwaka 2009.

Ustaz Yusuf alikuwa na wake wanne na watoto 12 miongoni mwao ni Abu Musab al-Barnawi ambaye alitoa taarifa za kifo cha Abubakar Shekau.

Tangu Shekau alipokikalia kiti hicho alikuwa katika sintofahamu na al-Barnawi. Mamlaka za Nigeria zilikuwa zikiamini kuwa Shekau aliuawa mnamo mwaka 2009 wakati wa mapigano makali dhidi ya Boko Haram.

Hata hivyo mnamo Julai 2010, Shekau alijitokeza katika mkanda wa video akithibitisha kuwa yeye ndio kiongozi rasmi wa Boko Haram. Mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kuwa amefariki dunia.

Mnamo Machi 2015, Shekau alitangaza muungano wake na kiongozi wa kundi jingine la Kiislamu la ISIL Abu Bakr al-Baghdadi. Shekau alikuwa muumini wa Kiislamu wa madhehebu ya Sunni katika tawi la Salafi hadi mwaka 2016, pale alipotamatisha uhusiano wake na ISIL.

Shekau anachukuliwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu hata kama aliona mara moja na kuwa na maono.

 

 

 

0 Comments:

Post a Comment