Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Monday, February 25, 2019

Rami Malek aweka rekodi ya kwanza Tuzo za Oscars 2019


Rami Malek anakuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya Uarabuni na Marekani kushinda tuzo ya Oscar 2019 katika kategori ya Mwigizaji Bora. Tuzo Hizo za 91 zilifanyika katika ukumbi wa Dolby Theatre,Hollywood, jijini Los Angeles nchini Marekani.
“Green Book won three awards, including Best Picture, and Bohemian Rhapsody won four awards, the most for the ceremony, including Best Actor for Rami Malek's portrayal of Freddie Mercury. Roma and Black Panther also received three awards, with the former winning Best Director for Alfonso Cuarón. Olivia Colman was awarded Best Actress for portraying Anne, Queen of Great Britain in The Favourite.”- According to https://en.wikipedia.org/wiki/91st_Academy_Awards


Sunday, February 3, 2019

RON W. DAVIS: Alivyopigiwa simu kutoka Tanzania-4



Makala yaliyopita tuliangazia namna kocha Ron Davis alivyoamka asubuhi mjini Edmonton na ndoto ya maisha yake kubadilika pale alipokutana na mwanariadha wa kwanza aliyeipa medali ya kwanza Tanzania Filbert Bayi na baadaye kocha Sulus.

Tukio hilo lilitokea mwaka 1978 kwenye michuano ya Jumuiya ya Madola ilifanyika mjini Edmonton, Alberta nchini Canada ambako Tanzania ilishiriki. Ron Davis alikuwapo Edmonton kama kocha wa Nigeria ambayo ilikacha kushiriki baada ya kutoka All Africa Games jijini Algiers. Katika makala haya tutaendelea na safari ya Ron Davis kilichofuata baada ya kupokea miadi kutoka kwa Kocha Sulus.

Ron Davis anasema, “ Sulus alinipigia simu siku chache baadaye na kuniambia kuwa Waziri wa Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Chadiel Mgonja anapenda kukutana na mimi.”

Wakati huo Ron Davis alikuwa bado kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, na tukio hilo lilimfanya sasa aanze kuwa karibu kwani hakutegemea kuwa ingeweza kuwa muujiza mkubwa wa yeye ambao ulikuwa akiusubiri kwa miaka mingi.

Ron Davis alijiuliza maswali mengi kwamba je asubuhi ile katika viunga vya Edmonton nchini Canada akimsemesha Bayi wakati akifanya mazoezi yake kama utani tu ndio imekuwa kitu kamili.

Ilimstaajabisha sana raia huyo wa Marekani. Aidha tukio hilo la kupigiwa simu liliweza kudakwa na magazeti ya Canada wakati ule kwani walikuwa wakimfahamu vizuri Ron Davis kwani aliwahi miaka ya nyuma kuwapo huko Alberta kwa kama mkurugenzi wa michezo.

MAZUNGUMZO NA GAZETI LA CANADA
Kukutana na Waziri Mgonja ilikuwa habari kubwa sana kwa wanahabari nchini Canada na waliomba kukutana naye kwa ajili ya mahojiano. Lakini Ron Davis anakiri kwamba mahojiano yale yalitaka kumtokea puani kutokana na kwamba alikuwa bado na kibarua na taifa la Nigeria.

Wanahabari walitaka kujua kutoka kwake sababu za Nigeria hatohudhuria michezo hiyo ya Jumuiya ya Madola mjini Edmonton. Ron Davis anasema, “Mojawapo ya vitu nilivyosema ilikuwa ni kwamba maofisa wa Nigeria ndio walioamua kutoshiriki michuano hiyo.”

Kwa taarifa yako jibu hilo lilitosha kujaa kwenye kurasa za magazeti ya Canada siku iliyofuata na kusomwa na watu wengi nchini humo. Ron Davis anasema alishindwa kumjibu mwandishi wa habari katika muktadha wa kisiasa.

Kwa muktadha wa kisiasa jibu lingekuwa siku zote Nigeria iko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya vitendo vya ubaguzi wa rangi na kukosekana kwao ni sehemu ya msimamo wa viongozi kuhusu vitendo hivyo.

Baada ya tukio hilo alikutana na Abraham Ordia ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Nigeria na Rais wa Baraza Kuu la Michezo barani Afrika. Ordia alimwambia kuwa hajapendezwa na baadhi ya kauli alizozitoa kwenye vyombo vya habari na kumtaka asizungumze tena na vyombo vya habari akiwa nchini Canada labda kwa makubaliano maalum.

Ron Davis anasema aliomba radhi kutokana na makosa hayo ambayo yalimfanya hata yeye mwenyewe ajisikie vibaya. 

AKUTANA NA CHADIEL MGONJA
Hatimaye siku iliwadia pale alipokutana na Waziri Mgonja. Ron Davis anasema, “Nilifurahi sana kukutana na Mgonja na ilipendeza sana.”

Katika mahojiano yao Ron Davis alijisemea moyoni endapo atafanikiwa kuajiriwa na serikali ya Tanzania utakuwa uhusiano ambao hautavunjika kamwe. Mafanikio aliyoyapata akiwa na Nigeria ilikuwa pointi muhimu ambayo ilimpa nafasi ya kuwa kocha wa Tanzania.

Mgonja alionyesha wazi kuwa alikuwa na mipango mikubwa kwa ajili ya Tanzania pale alipomwambia kuwa anamtaka Ron Davis kwa ajili ya kuwa kocha wa timu ambayo itashiriki michuano ya Olimpiki mwaka 1980. 

Katika mkutano wake na Mgonja kulikuwapo na mjumbe wa ubalozi wa Tanzania. Kila kitu kilifikiwa kuhusu uhamisho wake na namna ya kufanya kazi Tanzania. Ron Davis alitoa taarifa zake hali hiyo ilimfanya ajione kuwa anatembea angani kutokana na furaha isiyo kifani na tabasamu lililojaa matumaini makubwa ya kufanya kazi Tanzania.

Akiwa Edmonton alimshuhudia na alijua kuwa Bayi angekimbia fainali za mita 1500. John Carlos na rafiki zake waliungana naye kuona namna Bayi atakapofika kwenye kinyang’anyiro.

Ron Davis alimuona Bayi akianza kwa nguvu lakini katika mita 100 za mwisho Mwingereza Dave Morcroft alimburuza na kutwaa medali ya dhahabu na kusalia kuwa na medali ya fedha. Kitendo hicho kilimuuma sana Ron Davis, Carlos na wenzake kwani hawakutarajia kama angepitwa.

Wakiwa katika hali uchungu wa uwanjani zilikuja taarifa nyingine kuwa mke wa John Carlos alikuwa amefariki dunia, sasa hapo ikawa habari nyingine chungu zaidi na suala la Bayi likafutika kwenye vichwa vyao.

Ron alirudi Nigeria na kuaga vizuri kisha safari ya Tanzania ikaanza baada ya kupewa taarifa kwamba amechaguliwa kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa katika mbio za uwanja.

Alipotua Tanzania alishangazwa na umati wa wanahabari katika Uwanja wa Ndege wakimsubiri kwa shauku. Kilichomstaajabisha alikuwa hajawahi kuona hapo kabla. Ilikuwa ngumu kuamini kwani watu hawakuficha shauku na matarajio yao kwake katika medani ya riadha.

Makala haya yametayarishwa na Jabir Johnson ambaye alipata fursa ya kuzungumza na Ron Davis  katika masuala mbalimbali ya maisha yake na medani ya riadha alipotua nchini Tanzania. Kwa maoni ushauri barua pepe: jaizmela2010@gmail.com

Qatar yatwaa Kombe la Mataifa ya Asia 2019



Inaweza ikawa ngumu kuamini kilichotokea jijini Abu Dhabi katika mchezo wa fainali ya mataifa ya bara la Asia lakini ndivyo hali ilivyo pale miamba ya soka ya Asia Japan ilipoangushwa na Qatar kwenye mchezo ulichezwa kwenye dimba la Mohammed Zayed.

Japan iilishindwa kutwaa taji hilo kwa mara ya tano baada ya kuzabuliwa kwa mabao 3-1 na hivyo Qatar kutawazwa mabingwa wapya wa Mataifa ya Asia mwaka huu. Qatar ambao watakuwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2022 wameweka rekodi waliyoshindwa kuiweka kwa takribani miaka 63 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo. 

Mabao ya Almoez Ali, Abdelaziz Hatim na Akram Afif yaliamua kipute hicho cha soka Februari Mosi. Pia zawadi wa ufungaji bora ilikwenda kwa Almoez Ali akifikisha mabao tisa kwenye mi chuano hiyo. 

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 anayehudumu katika klabu ya Al Duhail alifunga katika dakika ya 12 ya mchezo bao la tisa baada ya juhudi na kumwacha mlinda mlango wa Japan Shuichi Gonda akisalia hana msaada.