Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Thursday, August 12, 2021

Chifu Mwariko ataka chanjo ya Uviko-19 iende kwa wanyamapori


Chifu Athumani Omary Mwariko 'Mhelamwana'

Chifu Athumani Omary Mwariko 'Mhelamwana' ameishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuangalia upya namna ambavyo wanaweza kupambana na janga la Covid-19 kwa wanyamapori ili kuzuia maambukizi mapya ya virusi hivyo.

Hayo yanajiri wakati serikali ikiendelea na utoaji wa chanjo ya maradhi hayo katika mikoa mbalimbali nchini huku sintofahmu ikitawala miongoni mwa jamii licha ya hiari kuwepo kwa anayetaka kuchanjwa.

Akizungumza na gazeti LaJiji Chifu Mwariko alisema virusi vilivyo vingi vimekuwa vikisambaa kupitia wanyama kisha kuingia katika mwili wa binadamu na kusababisha madhara makubwa.

“Virusi vimekuwa hatari sana kwa binadamu, kwani vilivyo vingi vimekuwa vikianzia kwa wanyamapori kisha kusambaa kwetu, nafikiri na ninatoa ushauri kwa serikali kuona namna ambavyo wanaweza kutoa chanjo hata kwa wanyamapori,” alisema Chifu Mwariko.

Chifu Mwariko kutoka katika jamii ya Waseuta wa Kizigua alisema utalii ni muhimu katika mbuga zetu kwani umekuwa kitovu cha uchumi wa Tanzania hivyo tahadhari ni vema zikachukuliwa ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kutoa matunda yanayokusudiwa.

“Tumekuwa tukiitegemea sekta ya utalii, tuna mbuga za wanyama ambao nao uchunguzi ukifanywa kwa weledi itatusaidia kudhibiti janga hili kwani wanyama pori wamekuwa chanzo cha virusi kukaa nao wakipata itaondoa hofu kwa watanzania,” aliongeza.

Aidha Chifu Mwariko ambaye ni msanii wa kitaifa na kimataifa na anayejihusisha na masuala ya kimila aliendelea kupongeza juhudi ambazo Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuzichukua kuhakikisha nchi haitetereki katika kipindi hiki ambacho ulimwengu unazidi kutoa machozi.

“Shukrani nyingi zenye furaha na amani tushukuru tumejiwa na mgeni mwema mzuri na tulikuwa tunategemea miaka mingi tupate Rais mama katika nchi yetu ya Tanzania na tumeshapata na tunafurahi na tunaunga mkono sasa. Ni mmoja katika wamama wa aina yake na pia  katika bara la Afrika hata ulimwengu  mzima sisi tunashukuru tumepata kiongozi mwenye busara na mwelewaji kama Mama Samia Suluhu Hassan,” anasema Chifu Mwariko.

Majuma kadhaa yaliyopita Serikali ilieleza kuwa mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza imekuwa hatari kwa maambukizi na vifo vya watu walioambukizwa kirusi cha Delta, wimbi hilo la tatu ambalo limezua taharuki dunia.

Kanuni ya Cashflow Quadrant: Kwanini wazazi wanataka watoto wasomee Sayansi, Hesabu na Sheria


 Kanuni ya Cashflow Quadrant,

Cashflow Quadrant hii ni kanuni ya kuwapanga watu kutokana na namna wanavyopata pesa au kwa kifupi umepata pesa kutokana na mfumo upi. Kulingana na Robert Kiyosaki mwanzilishi wa kanuni hiyo anawapanga watu katika makundi manne kwa alama nne E, S, B na I . Kanuni hii inaweka bayana kwanini baadhi ya watu wanafanya kazi kidogo, wanalipa kodi kidogo na wako salama katikamasuala ya kiuchumi kuliko wengine. Pia katika kanuni hii utabaini kuwa, kwanini katika Zama za Mapinduzi ya Viwanda (Industrial Age), wazazi wengi waliwataka watoto wao kuwa madaktari, wahasibu au wanasheria na kwanini katika Zama za Utandawazi, taaluma hizo zinajikuta katika wakati mgumu kifedha?

Kundi la kwanza: E

E inasimama badala ya Employment. 

Kundi la pili: S

S inasimama badala ya Self Employment.

Kundi la tatu: B

B inasimama badala ya Bussiness.

Kundi la nne: I

I inasimama badala ya Investiment.