Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Sunday, November 20, 2016

Guninita atoa rai Chadema

NA MWANDISHI WETU
John Guninita
 MAKATIBU wa Wilaya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wametakiwa kujenga utaratibu wa kuwaita makatibu wakuu wa kata katika wilaya zao na kuwapa taarifa za mapato na matumizi ili kurahisisha utendaji wa chama bila manung’uniko.
Katika mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa wilaya hiyo Bernard Mwakyembe walihudhuria Mbunge wa Viti Maalum jimbo la Temeke Lucy Magereri, Afisa Kanda ya Pwani kwa tiketi ya chama hicho Christopher Mbusule Shiru
Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo Chang’ombe jijini Dar es Salaam kiongozi huyo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema mapato na matumizi katika chama ni sehemu nyeti ambayo isipowekewa utaratibu mzuri huibua migogoro isiyo na sababu.
Aidha Guninita alisisitiza serikali ya Rais John Magufuli (JPM), imejaa woga, kiburi na majivuno yasiyo na msingi wowote katika maendeleo ya nchi hii.
“Mimi ni mwanasiasa wa siku nyingi…viburi, majibu ya hovyo hovyo, hiyo ndiyo CCM ya sasa. Rais ni kama mpiga ngoma anapiga mwenyewe na kutaka kucheza mwenyewe… Haiwezekani,” alisema Guninita.
Pia aliongeza tatizo kubwa la watanzania namba moja ni maji na kwamba Rais anaogopa kukosolewa juu ya hilo.
“Rais mzuri ni yule anayewaruhusu wananchi wake wamkosoe, sio yule anayefanya tathmini kwa mwaka mmoja…hatujaona mabadiliko kwa Magufuli,” alisema Guninita.
Kwa upande wake Magereri alisema Operesheni Amsha Chama inakuja na itaendeshwa nchi nzima kuelekea 2020 na kuongeza kadi mpya za kielektroniki kwa wanachama zitaanza kupatikana mwaka ujao.
Aidha Afisa wa Kanda ya Pwani aliwataka wanachama wasitishike na vitisho vya serikali iliyopo sasa isipokuwa sauti ya pamoja itatwatoa katika konga hilo.
Pia aliwataka wanasheria wa chama kupita katika kata na kuwaeleza na kutolea ufafanuzi wa katiba ya chama chao ili kuongeza na kukuza uelewa wa mwongozo huo hali itakayoondoa sintofahamu.
Kata 13 za wilaya ya Temeke zilihudhuria mkutano huo hivyo kutimiza akidi kwa mujibu wa Sura ya sita (6.2), ya katiba ya chama hicho 
Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bernard Mwakyembe (katikati) akipiga makofi pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya hiyo uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mwenezi wa Wilaya hiyo Edson Joel, kulia ni mgeni rasmi John Guninita. (Picha na Mpigapicha wetu





Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lucy Magereri akizungumza jambo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam.




Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Lucy Magereri akizungumza jambo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika jana Chang’ombe jijini Dar es Salaam.